- Watu kujifunza namna ya kujiendeleza kielimu na kuendesha biashara mtandaoni
Hatua hii ni miongoni mwa utekelezaji wa kampeni ya ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ awamu ya pili, ambayo pamoja na mambo mengine ina lenga kutoa elimu kwa wakazi wa Zanzibar juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G katika kuleta maendeleo ya kijamii na uchumi.
Mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Zantel wa kuchochea mageuzi ya kimtandao na kufanya watu waishi kidigitali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Zantel-Zanzibar, Rukia Mtingwa alisema kuwa kituo hicho cha Kiditali kitatoa huduma za kimtandao bure kwa wakazi wa Zanzibar ndani ya miezi miwili.
“Sehemu hii ina wataalamu na wabobezi wa huduma hizo za Elimu na Biashara za mtandaoni ambao watakuwa wakitoa mafunzo kwa watu watakaofika hapa, namna ya kutumia mtandao wa 4G kupata huduma hizo,” alisema.
“Elimu ya mtandaoni si kwa ajili ya wanafunzi wa shule na vyuo tu, bali hata kwa watu wenye vipaji mbalimbali na wafanya biashara wanaweza kujifunza kupitia mtandao namna bora ya kukuza na kutangaza kazi zao na kuboresha. Kwa mfano leo hii tuko na Said Sugu ambaye yeye ameweza kutengeneza magari, helikopta kwa kutumia kipaji chake na mtandao kuongeza ujuzi,” alisema
Wafanya biashara pia wana fursa ya kupata masoko mapya mtandaoni. Wakiwa hapa katika kijiji cha kidigitali, watafundishwa namna rahisi ya kutumia mitandao kuuza na kutangaza biashara zao.
Pamoja na hilo, Zantel imezindua shindano la kidigitali ambalo linatoa fursa kwa watu mbalimbali kuonesha vitu ambavyo wamejifunza na kutengeneza kwa kutumia mtandao na kujishindia zawadi hadi Sh300,000.
“Unachotakiwa kufanya ni kutengeneza video fupi na kuipost kwenye mtandao wa kijamii na kutag kurasa za Zantel.Video ambayo itapendwa zaidi itajishindia zawadi hadi Shilingi 300,000,” alisema.
No comments:
Post a Comment