Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 30 October 2018

VODACOM YAHIMIZA MICHEZO KWA WAFANYAKAZI WAKE - SPORTS BONANZA

KAMPUNI ya mawasiliano Vodacom Tanzania imehimiza wafanyakazi wake pamoja na jamii kuzingatia michezo ili kuweza kuimarisha utendaji kazi pamoja na ubora wa afya kwa manufaa binafsi na manufaa ya taifa kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa kazi Vodacom Bi. Karen Lwakatare wakati wa siku ya Vodacom Sport Bonanza day iliyofanyika Jumamosi katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam.

"Tunafanya bonanza kwa ajili ya wafanyakazi wote wa Vodacom kuhamasisha mazoezi kwa afya ya wafanyakazi na jamii kiujumla. Mshindi atakayepatikana atapata fursa ya kwenda kushiriki mashindano ya Vodacom Wellbeing Challenge ya mwaka ambayo hufanyika nje ya nchi yanayowakutanisha wafanyakazi wa Vodacom na Vodafone duniani” Lwakatare aliongeza.

Bonaza hilo limehusisha michezo ya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, kukimbia, kuogelea, gofu, tenesi, Volley ball, kuruka kamba, draft, rede kutembea kwa miguu na kuendesha baisikeli kutoka ofisi za makao makuu ya Vodacom hadi Gymkhana.


Kundi la waendesha baiskeli wakishangilia baada ya kuwasili viwanja vya Gymkhana kutokea makao makuu ya kampuni ya Vodacom, Jumamosi wakati wa siku ya Vodacom Bonanza iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana.
Glory Mtui akiongoza mbio za baiskeli kutoka makao makuu ya ofisi za Vodacom kuelekea viwanja vya Gymkhana jana wakati wa Sports Bonanza ya kampuni ya Vodacom.
Sandra Oswald akiongoza mbio za baiskeli kutoka makao makuu ya ofisi za Vodacom kuelekea viwanja vya Gymkhana jana wakati wa Sports Bonanza ya kampuni ya Vodacom. 
Mwanandada Naaja akiwaongoza wafanya kazi wa Vodacom Tanzania kwenye mazoezi ya viungo jana katika viwanja vya Gymkhana.
Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom wakifanya mazoezi ya viungo jana katika viwanja vya Gymkhana kuadhimisha siku ya Vodacom Sports Bonanza.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishindana mchezo wa kuogelea katika viwanja vya Gymkhana wakati wa maadhimisho ya Vodacom Sports Bonanaza.

No comments:

Post a Comment