Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 31 October 2018

BENKI YA KCB TANZANIA YATOA MSAADA WODI YA WANAWAKE KATIKA HOSPITALI YA RUFAA AMANA

Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Mahusiano wa Benki ya KCB, Christine Manyenye (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye mkutano wa makabidhiano ya misaada mbalimbali ikiwemo vitanda 10, magodoro 10, mashuka 20, vyenye thamani ya shilingi 6,017,000 katika wodi ya wananwake Hospitali ya Amana Ilala Jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dr. Amim Kilomoni.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali Ya Amana, Dr. Amim Kilomoni (kulis) akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa makabidhiano ya misaada mbalimbali toka Benki ya KCB ikiwemo vitanda 10, magodoro 10, mashuka 20, vyenye thamani ya shilingi 6,017,000 kwa wodi ya wanawake katika Hospitali hiyo leo jijini Dar Es Salaam. 
Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Mahusiano wa Benki ya KCB, Christine Manyenye (kushoto) akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dkt. Amim Kilomoni moja kati ya Vitanda na Vifaa vingine vyenye thamani ya shilingi 6,017,000 kwa wodi ya wanawake Hospitali ya Amana, Dar Es Salaam.
Wafanyakazi wa KCB na wauguzi wa Hospitali ya Amana wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya Benki ya KCB kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 6,017,000 kwa wodi ya wanawake leo kwenye Hospitali ya Amana Ilala, Dar Es Salaam.
Dar es Salaam, 31 Octoba, 2018 – Benki ya KCB Tanzania imekabidhi msaada wenye thamani ya milioni 6 kwa wodi ya wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano Mkuu wa Masoko, Mawasililiano na Mahusiano wa benki hiyo, Christine Manyenye alisema kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo na uhitaji.

“Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Afya, Elimu, Mazingira, Ujasiriamali na masuala ya ubinadamu”, Bi. Manyenye alisema na kubainisha kwamba tangu benki hiyo ilipofungua milango yake hapa Tanzania mwaka 1997, imekuwa ikijikita katika kuisadia jamii.

Benki ya KCB ilikabidhi misaada mbalimbali ikiwemo vitanda 10 magodoro 10, mashuka 20, vyenye thamani ya shilling 6,017,000 katika Hospitali hiyo. Mkurugenzi huyo alisema kuwa upungufu wa vitanda, magodoro na masuka katika hospitali nyingi nchini ni changamoto hasa katika wodi za akina mama na watoto Benki ya KCB iliamua kutoa msaada huo ilikupunguza changamoto hizo.

Akitolea mfano wa michango iliyotolewa na benki hiyo katika kupunguza viwango vya vifo vya kinamama na watoto nchini, Manyenye alisema: “Kupitia miradi hiyo Benki ya KCB Tanzania imeshazisaidia hospitali zaidi ya 15 kwa kuzipatia vifaa tiba mbalimbali.”

Alizitaja hospitali hizo kuwa ni Muhimbili, Mwananyamala, Ocean Road Cancer Institute, Buguruni, Sinza, Amana, Temeke na Kituo cha Afya cha Njia (Dar es Salaam); Mt. Meru na Ngarenaro (Arusha); KCMC, St. Thomas na Mawenzi (Moshi); SDA na Makongoro (Mwanza); Hospitali ya Morogoro (Morogoro); Kivunge Cottage na Kituo cha Huduma za Afya Kombeni (Zanzibar) na Hospitali ya Mkuranga (Pwani).

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali Ya Amana, Dr. Amim Kilomoni aliishukuru KCB Bank kwa msaada waliotoa kwani utasaidia kupunguza changamoto zilizokuwa zinawakabili, ikiwamo uhaba wa vitanda, magodoro na mashuka.

Kuhusu Benki ya KCB

Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 250, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 12,000 wanaotoa huduma za benki saa 24 siku saba za wiki katika Afrika Mashariki. Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda.

KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima, KCB Capital na KCB Foundation.

Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba ,Buguruni, Oysterbay, Pugu jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main naTFA, Mwanza na Morogoro.

Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment