Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 23 June 2021

BENKI YA EQUITY YAZINDUA KADI YA MALIPO YA EAZZY CARD

Mkuu wa Biashara wa Equity Group, Polycap Igathe (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Equity Bank Tanzania, Esther Kitoka (kulia) wakionyesha mfano wa kadi mpya ya "Eazzy Card" iliyozinduliwa na benki hiyo Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkuu wa Biashara wa Equity Group, Polycap Igathe (kushoto) akishika kadi mpya "Eazzy Card" pamoja na viongozi wa Equity Bank Tanzania katika uzinduzi wa kadi hiyo mpya ya malipo uliofanyika Dar es Salaam hivi karibuni.
  • Kadi za malipo ya awali zinazowezesha malipo ya kidijitali
  • Huweza kufunguliwa kwa mteja na asiyemteja wa Benki ya Equity
  • Huwezesha malipo Masaa 24 kupitia POS, ATM, Wakala na njia ya mtandao
  • Haina makato
  • Ni rahisi kuijaza fedha kupitia Eazzy Banking, Wakala, Matawini na Huduma Fedha za Simu za mikononi.
  • Inaruhusa pia malipo ya haraka kwa njia ya kugusa “tap and go”
Dar es Salaam Tanzania, 22 June, 2021 – Benki ya Equity (T) leo wamezindua rasmi kadi ya malipo ya awali ijulikanayo kama “Eazzy card” ikiwa na lengo la kurahisisha malipo ya kiditali na nchini kupitia huduma za fedha jumuishi.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Serena, Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank (T) Robert Kiboti alisema, kuwa kadi hiyo ni ya malipo ya kabla, ambapo mmiliki anaweza kutumia kiasi cha fedha ambacho tayari amekiingiza na kukitunza katika kadi yake husika. “Kadi hii ni ya malipo ya awali hivyo inaruhusu kuwa na matumizi mengi ikiwemo kulipia ankara au bili, kununua bidhaa, kutoa pesa kwenye mashine za ATM na pia kufanya malipo ya mtandaoni.”

Kiboti alisema kuwa kufuatia kuzinduliwa kwa kadi hizo, kutawezeshan hata watu wenye kipato cha chini kutunza fedha zao kwa urahisi na kujiwekea akiba kwa kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima. Alifafanua kwamba sasa wananchi wanaweza kupata kadi za Eazzy card kupitia Wakala wa Benki ya Equity au kupitia matawi ya Benki hiyo.

Pia ameeleza kuwa watanzania wengi wameonesha hamasa ya malipo ya kidigitali hivyo watahakikisha huduma hizo za kufanya malipo kwa njia ya mtandao zinawafikia wateja wao na wana malengo makubwa mbeleni katika kujenga uchumi wa nchi hasa kwa kwa kuzingatia sera ya nchi kwa sasa inayohamasisha na kuongeza kasi ua ukuaji wa malipo kwa njia ya kadi.

Akizungumzia juu ya faida ya kadi hizo Kiboti alisema kuwa zinamuongezea mteja au asiye mteja uwezo wa kufanya manunuzi pasipo kuwa na haja ya kubeba pesa taslimu. “Kadi ambazo kuzipata sio lazima uwe mteja wa Benki ya Equity, pia ni rahisi kuziongezea salio kwa kupitia Wakala, Simu za Mikononi, matawini na kupitia huduma fedha kwa njia ya simu” alisema.

Naye Mkuu wa kitengo cha Malipo na Huduma mbadala wa benki hiyo Raph Ligalama ameeleza kuwa lengo la uzinduzi wa kadi hiyo ni pamoja na kurahisisha na kuwawezesha wateja na wasio wateja wao kufanya (miamala) kidijitali na hivyo kuwaondolea usumbufu.

Faida za Eazzy card kutoka Equity Bank

  • Rahisi kufungua (Unahitaji kitambulisho cha NIDA tu)
  • Hakika na salama
  • Imeunganishwa na mtandao wa Visa hivyo kuweza kutumika kokote duniani
  • Urahisi wa kufanya malipo kwenye maduka, vituo vya mafuta, mahosipitali Daladala na masokoni.
  • Huondoa ulazima wa kubeba fedha taslimu hivyo kupunguza hatari ya wizi au mahitaji ya chenji.
  • Rahisi kujaza fedha
  • Inatumia kokote duniani
  • Uwezo wa kuchukua pesa taslimu inapobidi (kupitia Wakala, ATM au tawi)
  • Uwezo wa kufanya malipo ya mtandaoni

No comments:

Post a Comment