Cheti cha ISO 9001 ni uthibitisho kwamba kampuni imekidhi vigezo vya usimamizi wa ubora kwa mujibu wa mfumo wa usimamizi unaokubalika kimataifa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi cheti hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Davis & Shirtliff Tanzania, Benjamin Munyao alisema “Katika moja ya misingi yetu ‘Core Values’ ni ubora, kwahiyo cheti hiki ni msisitizo wa ubora wa wafanyakazi wetu, vifaa vyetu na utendaji kazi kwamba upo katika viwango vya juu sana.”
Alisema kupitia hatua hiyo, kampuni inaweza kufanya kazi kitaifa na kimataifa kwakuwa mashirika mengi yanahitaji kufanya kazi na kampuni ambazo zimethibitishwa na ISO.
“Kwa zaidi ya miaka 20 tumekuwa tukiendesha biashara hapa Tanzania kwa kuhakikisha tunatumia rasilimali watu, teknolojia na rasilimali mbalimbali kuboresha maisha ya watu kupitia kutoa suluhisho mbalimbali za kudumu kwenye sekta ya maji,” alisema.
Aliongeza kuwa lengo la muda mrefu ni kuhakikisha wanaleta matokeo chanya kwa jamii ili kuhakikisha rasilimali maji inatumika kwa ufanisi ili kudumu kwa vizazi vijavyo.
Davis and Shirtliff ni kampuni inayoaminika katika utengenezaji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali za maji nchini Tanzania na Serikali ikiwa mmoja wa wateja wake wakubwa.
Ni dhahiri kuwa, uwepo wa wazalishaji wa bidhaa ndani ya nchi ambao wanatambulika kimataifa ni jambo muhimu kwa maendeleo ya Taifa kwasababu inaokoa mud ana kupunguza gharama za kuagiza bidhaa nje ya nchi zinazohitajika kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Akikabidhi cheti hicho, Ofisa wa kampuni ya Bureau Veritas, Charles Vunugulu alisema kampuni hiyo imetimiza vigezo vyote ikiwamo kupitia mafunzo mbalimbali ya namna bora ya uendeshaji wa kampuni.
“Tutakachokifanya ni kuhakikisha kila baada ya mwaka tunafanya ukaguzi ili kuhakikisha kuwa kampuni inaendelea kuwa bora kila mwaka,” alisema.
Kampuni ya Davis & Shirtliff inazalisha na kusambaza bidhaa mbalimbali ikiwamo pampu za maji, majenereta, mabwawa ya kuogelea, mashine za kutibu maji pamoja na mashine za umwagiliaji kwneye kilimo.
No comments:
Post a Comment