Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 30 October 2019

VODACOM TANZANIA PLC NA MFUKO WA UBUNIFU WA HDIF WATEMBELEA HUBS MBALIMBALI KUJIONEA MAMBO MAKUBWA YANAYOFANYWA NA VIJANA NCHINI

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Hisham Hendi (wa tatu kutoka kulia) wakimsikiliza Adam Mbyallu wa Sahara Ventures walipotembelea Hubs za Sahara Ventures, DTBI, Jenga Hub na Seedspace zote za jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo iliandaliwa na mfuko wa ubunifu (HDIF) unaojishughulisha na kukuza ubunifu na kusaidia wabunifu nchini (Innovation ecosystem).
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi akichangia mada wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipofanya ziara ya kujifunza katika ofisi mbalimbali za uvumbuzi (innovation hubs) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Adam Mbyallu wa Sahara Ventures. Ziara hiyo iliandaliwa na mfuko wa ubunifu (HDIF) unaojishughulisha na kukuza ubunifu na kusaidia wabunifu nchini (Innovation ecosystem). 
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakimsikiliza Iddy John wa atamizi ya DTBI wakati akifafanua juu ya uvumbuzi wa Teknolojia unaoweza kuwaunganisha wafanyabiashara kwa pamoja wakati wafanyakazi wa vodacom walipofanya ziara ya kujifunza katika Hubs za Sahara Venture, DTBI, Jenga na Seedspace zote za jijini Dar es Salaam. 
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Hisham Hendi (wa pili kushoto) wakimsikiliza Andrew Tesha wa atamizi ya DTBI wakati akifafanua juu ya uvumbuzi wa Teknolojia inayoweza kuwaunganisha wafanyabiashara kwa pamoja wakati wafanyakazi wa vodacom walipofanya ziara ya kujifunza katika Hubs za Sahara Venture, DTBI, Jenga na Seedspace zote za jijini Dar es Salaam. 
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia (kulia aliye kaa) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Jenga Hub, Nancy Sumari (kushoto) wakati alipokuwa akifafanua jinsi walivyofanya uvumbuzi wa kuwafundisha watoto wa shule kwa kutumia Teknolojia (Innovation).
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia (wa pili kulia aliyekaa) wakimsikiliza meneja wa Hub ya Jenga Lupyana Mbembati wakati alipokuwa akielezea namna wanavyotumia Teknolojia kuwafundisha watoto wa shule wakati wafanyakazi hao walipofanya ziara ya kujifunza katika Hubs za Sahara Venture, DTBI, Jenga na Seedspace zote za jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Seedspace, Innocent Mallya akifafanua juu ya uvumbuzi wa Teknolojia inayowaunganisha wafanyabaishara (Innovation ecosystem in Tanzania) kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, wakati walipofanya ziara ya kujifunza katika Hubs za Sahara Venture, DTBI, Jenga na Seedspace zote za jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment