Kaimu Afisa Mkuu - Tigo Pesa, Angelica Pesha akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Tigo Pesa Mastercard QR, Jijini Dar Es salaam. |
Kaimu Afisa Mkuu - Tigo Pesa, Angelica Pesha akionesha kwa waandishi wa habari jinsi ya kulipia kwa Tigo Pesa Mastercard QR, katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Tigo Pesa Mastercard QR. |
Dar es Salaam. Oktoba 29, 2019 - Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kwa kushirikiana na Mastercard wamezindua kampeni kwaajili ya kuwazawadia wateja wanaofanya malipo kwa njia ya Tigo Pesa Mastercard QR katika maduka na maeneo yanayoruhusu kulipa kwa Mastercard QR.
Kampeni hiyo imelenga katika kuhakikisha wateja wanapata huduma rahisi na ya uhakika nchi nzima.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Kaimu Mkuu wa huduma za fedha (MFS), Angelica Pesha alisema “Kama kampuni ya kidigitali siku zote tunalenga kuleta sulushisho na kufanya maisha ya wateja wetu kuwa rahisi zaidi. Kumekuwa na ongezeko la uhitaji wa njia mpya na salama ya malipo kwa wateja pale wanapotaka huduma na bidhaa kwenye maduka na maeneo mengine ya kibiashara yanayoruhusu mfumo wa Mastercard QR.”
Aliongeza, “Tigo Pesa Mastercard QR ni fursa ya kuchochea agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi kwasababu Tigo Pesa ni huduma kamili ya kifedha. Kwa kupitia Tigo Pesa Mastercard QR si tu tunapanua wigo wa utoaji wa huduma zenye usalama kwa wateja bali tunasogeza huduma zenye uharaka karibu na wateja wetu,” alisema Pesha.
Mkurugenzi na Meneja wa Mastercard Afrika Mashariki, Frank Molla alisema “Mastercard imejizatiti katika kutafuta njia mbadala ya kifedha kwa kuja na suluhisho linatoa nafasi kwa wateja kupata huduma za malipo zenye usalama na za uhakika. Shabaha hii ya kuleta mbadala wa fedha ni jambo la kujivunia hasa tunapoungana na Tigo.”
Aliongeza “Kwa sasa biashara nyingi zinapokea malipo ya Mastercard QR ambapo wateja wanaweza kutumia njia hii ya kidigitali kujipatia zawadi ya fedha kwa malipo waliyofanya.”
Mteja wa Tigo anaweza kufanya malipo kwa njia ya Mastecard QR kupitia App ya Tigo Pesa kwa kuscani QR code au kwa kufuata hatua zifuatazo:
- Piga *150*01#
- Chagua namba 5
- Chagua 2, (Lipa kwa Mastercard QR)
Mastercard QR ni njia ya haraka na ya kidigitali yakufanya malipo ambayo kwa sasa inakubalika katika maeneo mbalimbali ya kibiashara kwa wateja wote wa Tigo Pesa.
Mteja anaweza kufurahia huduma ya Tigo Pesa Mastercard QR katika maeneo maarufu kama vituo vya mafuta vya Puma, migahawa ya KFC, Pizza Hut na Samaki Samaki, Century Cinemax, Supermarket ya Shoppers, JD Phamacies pamoja na maduka ya GSM Mall.
No comments:
Post a Comment