Applikesheni ya VSOMO ambayo inaendeshwa na kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania kwa kushirikiana na VETA imetaja kuwa moja ya soluhisho ya Tanzania kuelekea kuwa nchi ya viwanda.
Hayo yamesemwa na mkufunzi wa Tehama wa chuo cha VETA Kipawa Abdul Mollel wakati wa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakipata mafunzo ya ufundi kupitia applikesheni ya VSOMO ambayo inalenga kuwawezesha vijana nchni kujiendeleza kielimu kupitia application ya VSOMO kwa kupata masomo ya ufundi stadi ya VETA kupitia simu zao za mkononi ili kuongeza ujuzi wao.
‘Tunao wanafunzi wengi hapa Tanzania ambao wangetaka kupata elimu ya VETA. Wengine wako huko vijijini ambao huduma zetu hazipatikani. Lakini hata hivyo inakuwa ni vugumu kwa wao wote pamoja kupata nafasi hapa kwetu. Hata hivyo, kwa kupitia Applikesheni ya VSOMO imekuwa ni rahisi kutimiza azma yao, alisema Mollel.
Ili kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa viwanda, ni muhimu kuwa na wataalam wengi wenye elimu ya ufundi stadi. Huu mradi umekuwa ni muhimu sana kwani hata wale ambao hawana nafasi ya kuhudhuria mafunzo ya darasani wanayo nafasi ya kusoma, aliongeza Mollel.
Wanafunzi wanapata mafunzo kupitia simu zao za mkononi. Baada ya hapo ndio wanakuja hapa kwa ajili ya mafunzo ya vitendo. Wengi hapa leo wanafanya mafunzo ya ufundi umeme, simu na kompyuta. Kitu kikubwa tumeona ya kuwa vijana wanapata mafunzo kwa haraka lakini kikubwa wanakosa kujiamini. Sisi kama waalimu ndio kitu kikubwa kwanza tunakifanya, aliongeza Mollel.
Mafunzo ya vitendo yanachukua takriban masaa 60 baada ya hapo tutawapa mtihani wa mwisho pamoja vyeti. Ni vyema kwa vijana wengine huko mitaani kujiunga na applikesheni hii kwani itawaongezea ujuzi na ufanisi zaidi, aliongeza Mollel.
Akiongea wakati mafunzo hayo ya vitendo yakiendelea, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema kuwa Airtel imeamua kushirikiana na VETA kutoa mafunzo ya ufundi stadi kupitia applikesheni ya VSOMO baada ya kungundua ya kwamba kuna vijana wengi mtaani ambao wana nia ya kupata mafunzo hayo lakini wanakosa nafasi ya kuhudhuria darasani.
‘Tunatambua kwa Watanzania wengi ambao wana nia ya dhati kabisa kujiunga na VETA lakini wanakosa nafasi ya kuhudhuria darasani. Kupitia VSOMO ni fursa kwao kupata mafunzo kwa njia rahisi na nafuu. Pia tunatambua ya kwamba serikali imedhamiria kufanya Tanzania kuwa uchumi wa viwanda. Kuwa na vijana wengi wenye ujuzi wa fundi stadi ni moja ya njia ya kufanikisha hilo, aliongeza Mmbando.
VSOMO imepata mafanikio makubwa tangu kuanzisha kwake kwani mpaka sasa kuna vijana zaidi ya 30,000 ambao wamepakua applikesheni ya VSOMO kati yao 9,000 wamejiandikisha ili kusoma kwa mtandao. Tunatoa wito kwa watanzania hususani vijana kuchangamkia fursa hii kwa kupakua application ya VSOMO kwenye simu zao na kusoma kozi hizi za ufundi ambazo gharama yake ni 120,000/= hadi kumaliza na kupata cheti, alisema Mmbando.
Kozi zinazopatikana katika application ya VSOMO ni pamoja ni Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta,umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa magari. Vilevile Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.
No comments:
Post a Comment