Benki ya NMB imesaidia ujenzi wa duka kubwa la dawa katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi kwa kuchangia kiasi kikubwa cha shs milioni 30. Duka hilo limejengwa na NMB kwa kushirikiana na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na limegharimu kiasi cha sh milioni 59. Hili ni duka la kwanza kudhaminiwa na Benki hiyo huku likikadiriwa kuhudumia vituo vya afya, Zahanati na Hospitali zaidi ya 516 katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma hasa kwa upande wa Wilaya ya Tunduru.
Ujenzi wa duka hilo ni hatua ya mwitikio wa Benki ya NMB kuunga mkono juhudi za Raisi Dk. John Magufuli kwa kuweka maduka ya dawa katika hospitali kubwa nchini ili kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi na kwa bei nafuu.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa duka hilo jana, Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Richard Makungwa alisema NMB ilivutiwa sana na mpango wa serikali kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na benki hiyo imeamua kuunga mkono juhudi hizo za kuhakikisha huduma bora na nafuu zinawafikia wakazi wa Ruangwa na mikooa ya jirani.
No comments:
Post a Comment