Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Wednesday, 24 December 2025

VODACOM YAENDELEA KUGAWA MAKAPU YA SIKUKUU MOSHI, YAADHIMISHA MIAKA 25 YA HUDUMA NCHINI

Moshi, Kilimanjaro – Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeendelea kuwagusa na kuwashukuru wateja wake kupitia kampeni maalum ya kugawa makapu ya sikukuu, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano na wateja wake katika msimu huu wa sikukuu.

Katika tukio lililofanyika jana mjini Moshi, Meneja Mauzo wa Vodacom wilaya ya Hai, Gallus Massama, alikabidhi kapu la sikukuu kwa mkazi wa Njoro mjini Moshi, Asia Iddy Kasimu, kama ishara ya shukrani na kuthamini uaminifu wa wateja kwa kampuni hiyo.

Kampeni hiyo ya kugawa makapu imekuwa ikiendelea katika mikoa mbalimbali nchini, ikilenga kusherehekea pamoja na wateja na kurejesha kwa jamii inayotumia huduma za Vodacom kila siku. Tukio la Moshi limekuwa sehemu muhimu ya juhudi hizo, likiwakutanisha wateja na wawakilishi wa kampuni katika mazingira ya furaha na mshikamano.

Mbali na kusherehekea msimu wa sikukuu, hafla hiyo pia imeandaliwa ikiwa ni sehemu ya hitimisho la maadhimisho ya miaka 25 ya Vodacom Tanzania tangu kuanza shughuli zake nchini. Katika kipindi hicho chote, Vodacom imeendelea kuwa mdau muhimu katika maendeleo ya sekta ya mawasiliano, uchumi wa kidijitali na huduma jumuishi kwa Watanzania.

Kupitia kampeni kama hizi, Vodacom inaendelea kuonyesha dhamira yake ya kuwa karibu na wateja wake, kusikiliza mahitaji yao na kushiriki nao katika nyakati za furaha, huku ikiimarisha kauli mbiu yake ya “Tupo Pamoja”.

No comments:

Post a Comment