Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Wednesday, 22 October 2025

SBL YAZINDUA “TZEE” – KIBURUDISHO CHA TAIFA NA FURAHA YA WATANZANIA

Dar es Salaam, 14 Oktoba 2025

Serengeti Breweries Limited (SBL) imezindua rasmi TZEE, kinywaji cha gin cha kizalendo kinachoakisi ubunifu, fahari, na umoja wa Watanzania. Kinywaji hiki kimetengenezwa hapa nchini katika viwanda vya kisasa vya SBL na kinabeba kauli mbiu “TZEE ni SISI” — ishara ya uzalendo na utambulisho wa taifa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi, alisema kuwa kuzinduliwa kwa TZEE ni hatua muhimu katika safari ya kampuni hiyo kukuza vinywaji vinavyoakisi utamaduni wa Tanzania.

“TZEE imezaliwa kutokana na roho ya Kitanzania — imetengenezwa na Watanzania, kwa ajili ya Watanzania. Ni zaidi ya kinywaji, ni alama ya umoja, ubunifu, na fursa za kiuchumi,” alisema Obinna.

 

Kwa mujibu wake, TZEE si tu kinywaji chenye ladha ya kipekee bali pia ni jukwaa la kuunga mkono ubunifu wa vijana kupitia muziki, sanaa, mitindo, na teknolojia ya kidijitali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko na Ubunifu wa SBL, Henry Esiaba, alisema TZEE ni zao la mawazo ya ndani na kielelezo cha utamaduni wa Kitanzania unaoendelea kukua.

“Tulitaka kunasa miondoko, fahari na utu wa Kitanzania ndani ya chupa. ‘TZEE ni SISI’ si maneno tu, bali ni wito wa umoja na sherehe ya utambulisho wetu,” alisema Henry.

Kupitia TZEE, SBL inaendelea kuimarisha nafasi yake kama kinara katika soko la vinywaji vikali, ikiwakilisha kizazi kipya kinachoona Tanzania kama taifa la ubunifu na maendeleo.


No comments:

Post a Comment