Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 25 September 2023

NMB JAMII BOND YAZINDULIWA, RIBA YA ASILIMIA 9.5



  • Uwekezaji unaoigusa jamii
25 Septemba 2023 - Leo, tumezindua programu ya muda wa kati (Multicurrency Medium Term Note – MTN) ya miaka kumi yenye jumla ya shilingi trilioni moja, na kufungua rasmi dirisha la uwekezaji wa toleo la kwanza la Hati Fungani ya NMB Jamii (NMB Jamii Bond).


NMB Jamii Bond ina dhamiria kukusanya fedha ambazo zitatuwezesha kutoa mikopo inayolenga kuleta matokeo chanya kwenye jamii kupitia miradi ya mazingira, miradi inayogusa wanawake na vijana, miradi inayolenga kuhakikisha usalama wa chakula, nyumba za bei nafuu, afya, elimu na miradi mingine mingi.


Taarifa kuhusu Hati Fungani ya NMB Jamii (NMB Jamii Bond):
  • Riba - Wawekezaji watapata Riba ya asilimia 9.5% kwa mwaka na italipwa mara nne kwa mwaka.
  • Kiwango cha chini cha uwekezaji - TZS 500,000.
  • Muda wa Uwekezaji - Miaka 3.
  • Ofa imefunguliwa 25 Septemba 2023 na itafungwa 27 Oktoba 2023.

Lengo letu ni kukusanya Shilingi Bilioni 75, huku Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ikiruhusu ongezeko la mpaka Shilingi Bilioni 25. Pia idhinisho la USD million 10 limetolewa, na kuruhusu ongezeko la mpaka USD milioni tano, jumla ikiwa USD milioni 15, itakayouzwa kwa mashirika na wawekezaji walioko nje ya Tanzania.


Uzinduzi huu umehudhuriwa na Msajili Wa Hazina - Bw. Nehemiah Mchechu, Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Dkt. Edwin Mhede; Afisa Mtendaji Mkuu wetu - Bi. Ruth Zaipuna; Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) –
CPA. Nicodemus Mkama; Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) - Bi. Mary Mniwasa; pamoja na wawakilishi kutoka taasisi za ndani na nje ya nchi.


Tembelea tawi lolote la Benki ya NMB au Mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam waliopewa leseni na CMSA, uanze kunufaika na uwekezaji huu unaoigusa jamii.

#NMBJamiiBond 
#NMBKaribuYako

No comments:

Post a Comment