Wasanii wa kikundi cha sanaa wakitoa burudani. |
Balozi wa Uingereza nchini Bi. Sarah Cooke na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd, John Ulanga wakifuatilia jambo.
|
Mwonekano wa Nembo (Logo) mpya ya kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL). |
“Nembo mpya ya SBL inasimama ikiwakilisha ubora, ubunifu, utaalaum, urafiki na kujiamini. Nembo hii pia inaonyesha kuwa kampuni yetu inatengeneza bia zake kwa viungo asilia,” Mkurugenzi mtendaji wa SBL Mark Ocitti aliwaambia wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa nembo hiyo mpya jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, nembo hiyo ni kielelezo cha historia pamoja na vipindi ilivyopitia kampuni hiyo kwa miaka yote tangu ikimiliki kiwanda kimoja kidogo cha kuzalisha bia jijini Dar es Salaam hadi kufikia kampuni kubwa inayomiliki viwanda vitatu vilivyopo Dar es Salaam, Moshi na Mwanza huku ikitoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 800.
Bia zinazozalishwa na SBL ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Kibo Gold, Guinness pamoja na Senator. Bia hizi zimefanikiwa kushinda tuzo mbali mbali za kitaifa na kimataifa kutokana ubora pamoja na ubunifu unaotumika kuzitengeneza. SBL pia inasambaza pombe kali zinazoongoza kwa ubora na mauzo duniani kama Johnnie Walker, Smirnoff, White Horse, Gordons, Baileys na nyinginezo.
IIkijulikana kama mdhamini mkuu wa timu ya taifa (Taifa Stars), SBL katika kipindi cha miaka 10 imetekeleza miradi 17 ya maji nchi nzima kwa kuchimba visima kwenye sehemu zenye shida ya maji na kuwawezesha watu zaidi ya milioni 2 kupata maji safi na salama. Kwa mujibu wa Ocitti, kampuni hiyo inashirikiana na Wizara ya Kilimo kuwasaidia wanafunzi wanaofanya vizuri kutoka familia za wakulima kupata elimu ya chuo kupitia ufadhili chini ya mpango wa SBL Kllimo-Viwanda Scholarship.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya SBL John Ulanga alisema nembo hiyo mpya inaakisi lengo jipya la ukuwaji wa kampuni hiyo na kuongeza kuwa SBL imewekeza Paundi za Uingereza milioni 14 katika shughuli zake na upanuzi. “Uwekezaji huu mkubwa, utasaidia kutengeneza ajira mpya zaidi, utaongeza mchango wa SBL kwenye kodi kwa Serikali,”alisema.
Tukio la uzinduzi lilifanywa na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa aliyeelezea kuridhishwa kwake na mchango wa SBL kwa uchumi wa nchi na kuahidi kuwa Serikali itandelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara kwa ajili ya malkampuni pamoja na biashara. Bashungwa alisema maboresho yanayaofanywa kwa sasa kwenye sera yanalenga kuondoa urasimu usio wa lazima kwa taasisi za umma ambao ni kikwazo kwa maendeleo na ukuaji wa boashara.
No comments:
Post a Comment