Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 15 December 2014

WANANCHI WAFURIKA KATIKA BANDA LA DEGE ECO VILLAGE, MLIMANI CITY, DAR ES SALAAM

Muuzaji kutoka Hifadhi Builders Ltd akiongea na mteja kuhusu mradi wa Dege Eco Village jijini Dar es salaam hivi karibuni.

Adam Jusab, Afisa Masoko akihojiwa na waandishi wa habari hivi karibuni na kulia kwake Bwana Nyenshile, Afisa Mauzo wa Hifadhi Builders.

Muuzaji kutoka hifadhi Builders Ltd akiongea na mteja na kufafanua juu ya mradi huu wa Dege Eco Village iliyopo Kigamboni.

Banda lililopo Mlimani City la Dege Eco Village jijini Dar es salaam.

Wananchi wa jiji la Dar es Salaam wamepata nafasi ya kutembelea banda la Dege Eco Village na kufahamu juu ya mradi huo wa makazi bora unaofanyika Kigamboni eneo la Ras Dege. 

Akizugumza na wananchi waliotembelea banda hilo Afisa Masoko wa Hifadhi Builders Ltd inayosimamia mradi huo Bw. Adam Jusab alisema kuwa mradi huo ni kwa ajili ya wananchi wanaohitaji makazi bora na mpaka sasa nyumba elfu mbili zimekamilika kati ya nyumba elfu saba. 


Mradi huo utajumlisha aina mbili ya nyumba yaani appartments na villas. Pia kutakuwa na huduma za shule, kituo cha polisi, maeneo ya burudani, kituo cha zimamoto na huduma za usafiri wa mabasi kwa uchache. 

Amesema kwamba mradi huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2018. Pia aliendelea kusisitiza kwamba kama sehemu ya mazimio ya mwaka 2015 wa Tanzania wanashuariwa kununua nyumba zilizo kwenye makazi bora kama mradi huu wa Dege Eco Village. 

Kwa kumalizia aliwataka wale wote watakayohitaji kuwasiliana nao kufika kwenye ofisi zao zilizo mtaa wa Azikiwe Posta pembeni ya Benki ya NMB au kutembelea kwenye mtandao wa Dege Eco Village, www.degeecovillage.com au ukurasa wa facebook www.facebook.com/degeecovillage.

No comments:

Post a Comment