Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 15 December 2014

BENKI YA NBC YAWAPIGA JEKI VIJANA NA KUWAKUMBUKA YATIMA

Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Rukia Mtingwa (kushoto) akitoa elimu kuhusu ujasiriamali na  baadhi ya vijana kutoka vyuoni  walio katika kambi maalumu iliyoandaliwa na kampuni ya  Maa Media kwa udhamini wa NBC mjini Bagamoyo, Pwani hivi karibuni. NBC ilitoa kiasi cha zaidi ya shs milioni 100 ambapo mbali na ujasiriamali vijana hao walifundishwa  pia madhara na jinsi ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya.

Meneja  Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter (kulia), akisalimiana na Meneja Miradi wa Kampuni ya Maa Media, Albany James   wakati yeye na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo,  Rukia Mtingwa (kushoto)  walipotembelea kambi ya vijana iliyoandaliwa na Maa Media ili kuwafundisha masuala ya ujasiriamali, madhara na jinsi ya kuepukana na matumizi ya madawa ya kulevya. NBC ilitoa kiasi cha zaidi ya  shs milioni 100 kwa ajili ya kambi hiyo iliyofanyika mjini Bagamoyo. Wa pili kushoto ni  Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Lekoko Furaha.

Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Rukia Mtingwa akifanya mahojiano na waandishi wa habari wakati uongozi wa benki hiyo ukitembelea kambi ya vijana iliyoaandaliwa na Maa Media kwa udhamini wa benki ya NBC.

Vijana  wakijiweka sawa kabla ya kuanza kwa mafunzo yao.

Meneja  wa Benki ya NBC Tawi la Njombe, Sady Mwang’onda (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa vyakula, sabuni, mafuta na vitu vingine kwa walezi wa kituo cha watoto yatima cha Imiliwaha ikiwa ni moja wa matukio kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani mjini Njombe hivi karibuni.

Meneja  wa Benki ya NBC Tawi la Njombe, Sady Mwang’onda akifanya mahojiano na vyombo vya habari mara baada ya  kukabidhi msaada wa vyakula, sabuni, mafuta na vitu vingine kwa walezi wa kituo cha watoto yatima cha Imiliwaha ikiwa ni moja wa matukio kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani mjini Njombe.

No comments:

Post a Comment