Foreign Exchange Rates

Equity Bank Advert_12 February 2026

CRDB Bank Advert_070325

Global Sanctions Compliance Masterclass

Tuesday, 3 March 2026

RAOMA NA VODACOM WAZINDUA MFUMO WA KIDIJITALI CHINI YA KAMPENI YA TWENDE ZETU DARASANI

27 Februari 2026 – Dar es Salaam, Tanzania

Taasisi isiyo ya kiserikali ya RAOMA Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya teknolojia na mawasiliano ya Vodacom Tanzania Plc wamezindua rasmi mfumo mpya wa kidijitali wa elimu unaoitwa SOMO, chini ya kampeni mpya ya Twende Zetu Darasani.

Mfumo wa SOMO umeundwa mahususi na Vodacom Tanzania Plc kwa lengo la kusaidia ufundishaji na ujifunzaji wa masomo yote kwa kuzingatia mtaala wa elimu wa taifa. Kupitia teknolojia hii, mwalimu mmoja anaweza kufundisha wanafunzi waliopo katika maeneo mbalimbali nchini kwa wakati mmoja.


Kuimarisha Ubora wa Elimu Kupitia Teknolojia

SOMO inalenga kuimarisha juhudi zilizopo katika sekta ya elimu kwa:

  • Kuunganisha shule na walimu kupitia teknolojia
  • Kutoa zana shirikishi kwa wanafunzi na walimu
  • Kuhakikisha elimu ya kisasa, yenye ubora na ya kidijitali inapatikana kwa kila mwanafunzi

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Prof. Ladslaus Mnyone, aliyemwakilisha Naibu Waziri wa Elimu Wanu Ameir Hafidh, alisisitiza umuhimu wa teknolojia katika kufikia malengo ya taifa.

Tukiwa tunaelekea kufikia Dira ya Maendeleo ya 2050 ya kuwa uchumi wa dola trilioni moja za Marekani, tunatambua kuwa elimu ndiyo msingi mkuu wa mafanikio hayo. Kupitia matumizi ya teknolojia ya kidijitali katika ufundishaji na ujifunzaji, tunaongeza fursa za elimu, tunaimarisha ubora wake na tunawaandaa watoto wa Kitanzania kuwa na maarifa na stadi zitakazochochea maendeleo ya taifa letu.

Napenda kuwapongeza RAOMA Foundation pamoja na Vodacom kwa ushirikiano huu muhimu. Mfumo huu umebuniwa na wataalamu wetu wa ndani kwa ajili ya kuwahudumia watoto wa Kitanzania – haya ni mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu.”


Ushirikiano wa Sekta Binafsi Kuleta Mageuzi

RAOMA Foundation inashirikiana na Vodacom Tanzania kuhakikisha ndoto za wanafunzi zinatimia kupitia matumizi ya teknolojia. Ushirikiano huu ni mfano halisi wa namna sekta binafsi inavyoweza kusaidia kuboresha huduma za elimu nchini.

Mkurugenzi wa RAOMA Foundation, Rahma Abdallah, alisema:

Tunaendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, TAMISEMI pamoja na wadau wengine wa maendeleo na sekta binafsi, ili kuhakikisha mfumo huu unafika kila shule na kufanikisha elimu bora kwa kila mwanafunzi.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Bidhaa za Biashara na Suluhisho wa Vodacom Tanzania Plc, Ali Z. Ali, alieleza kuwa ubunifu huo ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kuharakisha safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kidijitali.

Mojawapo ya malengo yetu ni kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali. Tumekuja na ubunifu wa mfumo huu utakaomwezesha mwalimu mmoja kufundisha shule kadhaa au idadi kubwa ya wanafunzi katika maeneo mbalimbali bila yeye kuwepo moja kwa moja katika kila eneo.”


Hatua Muhimu Kuelekea Elimu Jumuishi

Uzinduzi wa SOMO ni hatua muhimu katika safari ya Tanzania kuelekea elimu jumuishi, ya kidijitali na yenye ubora. Mfumo huu unalenga kuandaa kizazi chenye ujuzi wa kidijitali, chenye uwezo wa kushindana kimataifa na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Kwa hakika, kupitia kampeni ya Twende Zetu Darasani, RAOMA Foundation na Vodacom Tanzania wanafungua ukurasa mpya katika mageuzi ya sekta ya elimu nchini.



No comments:

Post a Comment