Morogoro: Msimu wa saba wa TCB Selous Marathon umeweka rekodi mpya baada ya kuvutia zaidi ya washiriki 10,000, jambo lililoifanya kuwa mojawapo ya matukio makubwa zaidi ya michezo mkoani Morogoro.
Akizungumza kuhusu mafanikio hayo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, amesema tukio hilo linaunga mkono juhudi za Serikali za kuhamasisha mazoezi, kuimarisha afya za wananchi na kuleta mshikamano wa kijamii.
Amesema marathon hiyo imeendelea kukua kila mwaka na kutoa fursa kwa makundi yote ya jamii, ikiwemo watu wenye ulemavu, kushiriki katika shughuli za michezo na kujenga umoja wa Watanzania.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Adam Mihayo, amesema udhamini wa benki hiyo katika marathon hiyo unalenga kukuza afya, utalii, utunzaji wa mazingira na fursa za kiuchumi,amesema kupitia tukio hilo, TCB inalenga kutangaza Hifadhi ya Selous, kuunga mkono juhudi za upandaji miti ambapo miti 2,000 tayari imepandwa na mingine 8,000 itapandwa, sambamba na kuhamasisha matumizi ya mifumo ya malipo ya kidijitali.
Mihayo ameongeza kuwa zaidi ya washiriki 10,000 waliojitokeza wamechochea shughuli za kiuchumi mkoani Morogoro, huku sekta za hoteli, usafiri, biashara ndogo ndogo na huduma mbalimbali zikiongeza mapato kutokana na ongezeko la wageni,aidha, amesema marathon hiyo imesaidia kutangaza mradi wa reli ya kisasa ya SGR na vivutio vya utalii vya Tanzania kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wao, washiriki wa marathon hiyo wameeleza kuwa mbio hizo si mashindano pekee bali ni sehemu ya kujenga afya na kuhamasisha maisha yenye mazoezi,wamesisitiza kuwa ushiriki wa wananchi katika matukio kama hayo unasaidia kupunguza magonjwa yasiyoambukiza na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha ustawi wa jamii,hukub TCB ikiahidi kuboresha zaidi maandalizi ya msimu ujao kufuatia mafanikio makubwa ya mwaka huu yaliyovuka matarajio.

.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)


No comments:
Post a Comment