Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 2 July 2024

KOBE MOTOR JAPAN KUONGEZA IDADI YA MAGARI YAKE SOKO LA TANZANIA

Mkuu wa Masoko (Head of Marketing) wa kampuni ya Kobe Motor ya Japan inayojishughulisha na uuzaji wa magari yaliyotumika kutoka Japan, Ken Aoki, akizungumza na mteja aliyefika katika banda la kampuni hiyo katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Kampuni hiyo imeanzisha utaratibu (leasing) ambapo mteja anaweza kulipa 35% ya gharama na kujipatia gari kutoka Japan huku kiasi kilichobaki akikilipa kwa miezi 12 hadi 24.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Kobe Motor inayouza magari yaliyotumika kutoka Japan, Victoria Ngomale (kulia akiwasikiliza wateja waliotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Kampuni hiyo imeanzisha utaratibu (leasing) ambapo mteja anaweza kulipa 35% ya gharama na kujipatia gari kutoka Japan huku kiasi kilichobaki akikilipa kwa miezi 12 hadi 24.
Mkuu wa Masoko (Head of Marketing) wa kampuni ya Kobe Motor ya Japan inayojishughulisha na uuzaji wa magari yaliyotumika kutoka Japan, Ken Aoki, akimsikiliza mteja aliyetembelea banda la kampouni hiyo katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Kobe Motor inayouza magari yaliyotumika kutoka Japan, Victoria Ngomale (kushoto) akimwelekeza jambo mteja aliyetembelea banda la kampouni hiyo katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Kampuni ya Kobe Motor ya Japan imesema itaendelea kujitanua zaidi katika soko la Tanzania kutokana na kukua kwa mahitaji ya magari ya aina mbali mbali kwa ajili ya mtumizi binafsi na ya kibiashara.

Ikiwa ni moja kati ya makampuni makubwa ya Kijapani yanayouza magari yaliyotumika kutoka Japan sehemu mbali mbali duniani, Kobe Motor tayari imeshauza zaidi ya magari 150,000 hapa Tanzania na sasa inalenga kuongeza uuzaji wa magari zaidi hapa Tanzania na eneo zima la Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kobe Motor Umar Ali, Tanzania ni moja kati ya nchi 10 zinazoongoza kwa soko la magari kutoka Japan ana kusema kuwa kampuni yake inaiona Tanzania kama soko muhimu.

“Lengo letu ni kuongeza uwepo wetu kwenye soko linalokuwa kwa kasi la Tanzania ambalo ni kitovu kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki,” alisema wakati akiongea na waandishi wa habari.

Akiongea kuhusu kampuni hiyo kuwa karibu na wateja wake alisema Kobe Motor inashiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam na kuwataka watu kutembelea banda la kampuni hiyo kwa ajili ya kupata ofa pamoja na kujishindia gari kutoka Japan kupitia bahati nasibu itakayoendeshwa viwanjani hapo.

Katika hatua nyingine, afisa mtendaji mkuu huyo alisema Kampuni ya Kobe Motor imezindua utaratibu wa wateja kulipa 35% ya thamani ya gari na kupewa gari la ndoto yao huku kiasi kilichobaki kikilipwa kwa kipindi cha miezi 12 au 24.

“Kampuni yetu inajivunia kuwa ya kwanza kuanzisha utaratibu huu utakaomwezesha mteja kupata gari la ndoto yake pasipo kulazimika kuwa na gharama zote za ununuzi wa gari,” alisema.

Aliongeza “katika dunia ya leo chombo cha uhakika cha usafiri ni muhimu na halikwepeki, kwa kutambua ukweli huu, Kobe Motor imekuja na aina mbli mbali ya magari ili na za gharama nafuu ili kumwezesha kila mtu kuwa na chombo cha uhakika cha usafiri,”

Alisema wafanyakazi wa Kobe Motor watakuwa katika viwanja vya Saba Saba kuwaelekeza wateja watakaokuwa wanaoagiza magari kwa mara ya kwanza taratibu za kufuata mpaka gari linapowafikia milangoni mwao.

No comments:

Post a Comment