Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 4 July 2024

BENKI YA CRDB YASHINDA TUZO YA UBORA WA HUDUMA YA ESQR 2024

Mkuu wa Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB, Yolanda Uriyo (wa pili kushoto) akipokea Tuzo ya Ubora wa Huduma ya mwaka kutoka kwa Michael Harris, Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Utafiti wa Ubora ya Ulaya (ESQR). Wanaotazama ni Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Tanzania Brussels, Vivian Rutaihwa (wa kwanza kulia), na Meneja Mwandamizi wa Uhakiki wa Ubora wa Huduma wa Benki hiyo, Mshindo Magimba.

Brussels, 30 Juni, 2024 - Benki ya CRDB imetunukiwa Tuzo ya Ubora wa Huduma kwa mwaka 2024 na Jumuiya ya Ulaya ya Utafiti wa Ubora (ESQR) katika hafla ya utoaji wa tuzo iliyofanyika katika hoteli ya Le Plaza katika jiji la Brussels, Ubelgiji.

Tuzo hiyo ilitolewa kwa kutambua jitihada za Benki hiyo katika kuboresha usimamizi wa ubora katika huduma zake zote. Tuzo ambazo zinafanyika kila mwaka zinatambua taasisi na mashirika ambayo yamewekeza katika huduma ubora kwa wateja katika sekta mbalimbali, ikiwamo sekta ya fedha kote ulimwenguni.

Benki ya CRDB imekuwa ikiwekeza kwa kiasi kikubwa katika mifumo ya utoaji huduma bora inayojumuisha teknolojia za kisasa ili kutoa uzoefu bora katika kila hatua ya safari ya mteja. Ushindi wa tuzo hii, unathibitisha namna gani Benki ya CRDB imekuwa mshirika mzuri kwa wateja na wadau wake, ikichangizwa na wafanyakazi wenye weledi mkubwa ambao wamekuwa wakiwapa wateja suluhisho bora na zinazoendana na mahitaji yao halisi.

Akizungumzia wakati wa hafala ya kupokea tuzo hiyo Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Yolanda Uriyo, alisema, "Mtazamo wetu kubuni njia bora za kuwahudumia wateja umekuwa ndio msingi wa mafanikio yetu ya katika nyanja ya huduma kwa wateja na usimamizi wa ubora. Tuzo hii ni ushahidi wa bidii ya timu yetu katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu.”

Aliongeza kuwa tuzo hiyo inaakisi maono ya kimkakati ya Benki ya CRDB chini ya mkakati wake mpya wa muda wa kati, 'Evolve,' unaojumuisha mipango mbalimbali ya huduma kwa wateja inayolenga kuboresha utoaji wa huduma. Mipango hii imeimarisha nafasi ya Benki ya CRDB katika soko huku ikiimarisha uhusiano na wateja na ufanisi wa kiutendaji.


Akizungumza kuhusu tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, alisema kutambuliwa na ESQR ni hatua muhimu inayosisitiza dhamira ya Benki katika ubora na umahiri katika shughuli zake zote. "Juhudi za timu yetu katika uvumbuzi na mbinu zinazomjali mteja zinaendelea kututofautisha katika sekta ya benki. Tunaendelea kujidhatiti katika kuinua viwango vyetu vya huduma na kutoa thamani endelevu kwa wateja na wadau wetu," aliongeza.

Mbinu bunifu zilizochangia tuzo hiyo ni pamoja na utekelezaji wa mifumo ya kidijitali ya maoni ya wateja kama vile misimbomilia (QR Code) na mfumo wa jumbe fupi (SMS), zilizopelekea kuwapa wateja njia rahisi za kutoa maoni na kuwezesha benki kushughulikia kwa haraka. Zaidi ya hayo, Benki hiyo imekuwa ikifanya tathmini za mara kwa mara za ubora wa huduma na utoaji wa bidhaa, kuhakikisha uboreshaji endelevu na kuvuka matarajio ya wateja.

Akiwa ameongozana na Ujumbe wa Benki ya CRDB, Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Vivian Rutaihwa, alitipongeza Benki ya CRDB kwa kushinda tuzo hiyo akisema inaleta sifa nzuri sit u kwa benki hata Taifa kwa ujumla, “Tunajisikia fahari kubwa kuona Benki ya CRDB inatambulika kimataifa kwa huduma ubora ikitoa taswira ya viwango vya huduma kwetu kama nchi. Tunatamani kuona taasisi nyingi zikifikia viwango hivi."


Naye Michael Harris, Mshauri Mkurugenzi Mtendaji wa ESQR, aliipongeza Benki ya CRDB kwa mafanikio yake na kubainisha, "Ushindi wa tatu wa Benki ya CRDB wa Tuzo ya Ubora wa Huduma ni kielelezo cha dhamira yake isiyoyumba ya ubora na ubunifu katika huduma za kibenki. Tunawapongeza kwa kujitolea kwao kuweka viwango vya ubora wa usimamizi."

Hii ni mara ya tatu kwa Benki ya CRDB kutunukiwa tuzo ya ubora ya ESQR. Tangu Januari 2024, Benki hiyo imepata tuzo kubwa 26, ikiwa ni pamoja na Benki Bora Tanzania katika Tuzo za Global Finance, Benki Bora ya Biashara Tanzania katika Tuzo za International Banker, Benki Bora ya Ubunifu wa Huduma Inayomjali Mteja Tanzania katika Tuzo za Global Brands, na Benki Bora ya Ubunifu Tanzania katika Tuzo za Gazette International.

Wednesday 3 July 2024

AFRICAN WOMEN LEADERS NETWORK TANZANIA GENERAL MEETING

Hon. Riziki Pembe Juma, Minister of Community Development, Gender, Elderly and Children Zanzibar.
Speaking at the event, Hon. Angellah Kairuki, Minister for Natural Resources and Tourism and Chair of the Generation Equality Forum National Advisory Committee.
UN Women Tanzania Acting Representative, Peterson Magoola.
  • African Women Leaders Network Tanzania and Stakeholders Equality Forum Stakeholders to Galvanize Commitment, Financing and Accountability for Women’s Economic Justice and Rights
July 2nd, 2024 - Dar es Salaam; The African Women Leaders Network (AWLN), in collaboration with the Government of the United Republic of Tanzania and UN Women, has convened the regional meeting to reflect on progress, galvanize commitment, and catalyse the energy, activism, and ideas of women's rights organizations and young people.


Bringing together over 200 participants from strategic government ministries, women's rights organizations, climate justice activists, young feminist women, women and girls with disabilities, international financial institutions, private sector representatives, young women leaders, media, and AWLN chapters across African countries, the meeting seeks to support the Government of Tanzania's efforts as a Generation Equality Forum (GEF) leader, strengthening accountability for delivering GEF commitments, accelerating the achievement of Sustainable Development Goals (SDGs), and implementing the Beijing Platform for Action, particularly in gender-responsive macroeconomic planning and financing initiatives.


Reflecting on the GEF Midpoint event hosted by UN Women in New York in September 2023, it provided an important opportunity to mobilize sustained attention and investment in gender equality as an accelerator for the SDGs. This event was particularly crucial at a time when women’s rights are increasingly under threat globally, and progress has stalled or reversed in more than 30 per cent of the SDGs worldwide.

JAMBOJET LAUNCHES NEW FLIGHT TO ZANZIBAR FROM MOMBASA


Mombasa, Tuesday, July 2, 2024 - Jambojet Limited has officially launched a new direct flight route from Zanzibar to Mombasa, Kenya, as part of a strategic investment in the aviation sector to bolster socio economic growth particular in tourism, trade, and culture aligning with East Africa Vision 2050.

The inaugural flight departed from Mombasa, Moi International Airport (MBA/HKMO) and arrived in Zanzibar Abeid Amani Karume International Airport (AAKIA), marked by a celebration attended by officials from the Embassy of Kenya to Tanzania, Government representatives of Tanzania & Kenya, and executives of Jambojet among others.


Starting immediately, Jambojet will operate flights on this route four times a week—Monday, Wednesday, Friday, and Sunday. Flights will depart Mombasa at 5:10 PM and arrive in Zanzibar at 6:05 PM, with a flight duration of 55 minutes.

“Jambojet is dedicated to delivering outstanding service at competitive rates. Our new route starts at 24,420 Kenyan shillings, (495,000 Tanzanian shillings) for a round trip. As a leader in low-cost aviation, we pride ourselves on our competitive fares and extensive network, enabling more people to travel across East Africa This route reflects our goal of making air travel accessible to everyone. ” said Mr. Karanja, Ndegwa, Chief Executive Officer Jambojet.

Using De Havilland Dash 8 400 aircraft capable of carrying 78 to 82 passengers, Jambojet completes the Zanzibar-Mombasa journey in under an hour, facilitating convenient connections to Nairobi, Dubai, Frankfurt, Milan, and other destinations.

"On behalf of the Kenyan government, I am delighted to be part of today's launch of this new route operated by our airline, Jambojet, from Zanzibar to Mombasa. This step is crucial not only in facilitating quick and affordable air travel but also in strengthening commercial, tourist, and cultural ties between Tanzania and Kenya. By enhancing connectivity, we are fostering development along the East African coast," said Issac Njenga, Kenya's Ambassador to Tanzania

Tuesday 2 July 2024

TAMISEMI: TUIGE MFANO WA CRDB BANK FOUNDATION KUTOA FURSA KWA VIJANA NA WANAWAKE


Dar es Salaam, Tarehe 29 Juni 2024: Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Adolf Ndunguru ameipongeza Taasisi ya CRDB Foundation kwa jitihada zake za kuwafungulia fursa vijana na wanawake na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kuongeza ujumuishi wa kifedha na kuharakisha maendeleo ya taifa.

Ndunguru ametoa wito huo alipofungua semina ya wajasiriamali wanawake na vijana iliyoandaliwa na Taasisi ya CRDB Bank Foundation na kufanyika makao makuu ya Benki ya CRDB.


“Ili kuwawezesha zaidi wajasiriamali wanawake na vijana, ni muhimu wadau wote wa maendeleo wakashiriki. Serikali pekee haitoweza kutatua changamoto zote zinazotukabili kwa kasi tunayoitarajia. Lazima tufanye kazi pamoja ili kujenga mazingira ambayo kila mwanamke na kijana anapata fursa ya kufanikiwa.

Niipongeze CRDB Bank Foundation kwa kuja na programu hii ambayo inalenga kuboresha biashara za vijana na wanawake kwa kuwapa mafunzo na ushauri wa namna bora ya kusimamia na kuendesha biashara zao, kuwapa mitaji wezeshi, na kuwaunganisha na masoko ya ndani na nje ya nchi,” amesema Ndunguru.

Katibu mkuu huyo pia ameusifu utaratibu wa CRDB Bank Foundation kushirikiana na vikundi na taasisi za uwezeshaji wa wanawake na vijana nchini katika sekta mbalimbali za maendeleo kwamba unawafanya wananchi wajione ni sehemu ya benki na wanawajibika kwa maendeleo yao binafsi baada ya kupewa kemkem zilizopo kuweza kujikwamua kiuchumi.


“Kitendo cha kuwafikia wanawake wajasiriamali zaidi ya 400,000 na kutoa mitaji wezeshi yenye thamani ya shilingi bilioni 10 ndani ya muda mfupi kinaonyesha ni kwa namna gani mmejipanga kuleta matokeo makubwa kwa jamii yetu. Nivipongeze pia vikundi na taasisi mnazoshirikiana nazo katika kutekeleza Programu ya Imbeju. Serikali tunajivunia tukiona tulizozipa kibali cha kuchochea ujumuishi wa kifedha kwa wananchi na kukuza ustawi wa jamii zinakitimiza malengo yake kwa ufasaha,” amesisitiza Ndunguru.

Katibu mkuu ametoa pongezi hizo baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Mwambapa kueleza kuwa malengo ya taasisi hiyo ni kutoa elimu ya fedha, kukuza ubunifu na teknolojia, kuwawezesha wajasiriamali kwa mtaji, kuongeza ujumuishi wa kifedha na kiuchumi ili kuboresha maisha ya vijana na wanawake.


“Najivunia kukujulisha kuwa CRDB Bank Foundation imeshatoa mafunzo kwa wanawake na vijana zaidi ya 400,000 sambamba na mitaji wezeshi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 10. Wajasiriamali hawa, licha ya kufunguliwa Akaunti ya Imbeju, wana fursa ya kuwa mawakala wa Benki ya CRDB, kupata bima ya mazao na mifugo, kufahamu masoko mapya ya huduma au bidhaa zao pamoja na kufanya biashara ya kimataifa kupitia mpango Eneo Huru la Biashara Huria la Africa (AfCFTA),” amesema Tully.

Ili kuwafikia wanufaika wengi zaidi, Tully amesema wanashirikiana na wadau wa ndani na wa kimataifa BUTA VICOBA Endelevu, Bunju Women Entrepreneurs (BWE), Mbweni Women Empowerment (MWE), Eden Group, UWABISORA, Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Tume ya TEHAMA (ICTC), Sokoine University Graduate Entrepreneurs Cooperative (SUGECO), pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).


Kabla ya kumkaribisha geni rasmi kuzungumza na zaidi ya washiriki 350 wa semina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki y CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema wanawake na vijana ni kundi lenye uwezo mkubwa wa kuliinua taifa kuondokana na umasikini ndio maana bodi ya wakurugenzi na menejimenti wameridhia kuelekeza nguvu kubwa kuwawezesha kushiriki kuujenga uchumi.

“Wanawake na vijana ni makundi yanayokabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi ndio maana Benki yetu ya CRDB kupitia CRDB Bank Foundation iliona kuna kila sababu ya kutoa elimu na kuwapa mitaji wezeshi wale wanaokidhi vigezo ili kujenga uchumi jumuishi na shirikishi ili kuwa na maendeleo endelevu,” amesema Nsekela.



Mkurugenzi Mtendaji wa Benki y CRDB, Abdulmajid Nsekela
akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wajasiriamali wanawake na vijana iliyoandaliwa na Taasisi ya CRDB Bank Foundation na kufanyika katika makao makuu ya Benki ya CRDB, mwishoni wa wiki.



Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Bank Foundation, Martin Warioba akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wajasiriamali wanawake na vijana iliyoandaliwa na Taasisi ya CRDB Bank Foundation na kufanyika katika makao makuu ya Benki ya CRDB, mwishoni wa wiki.





UZINDUZI WA MSIMU WA PILI WA MASHINDANO YA GOFU YA NCBA YAONGOZANA NA UPANDAJI MITI ARUSHA


Arusha, Tanzania - Juni 29, 2024: Benki ya NCBA Tanzania imezindua rasmi msimu wa pili wa mashindano ya gofu ya NCBA. Mashindano haya yalifanyika kwenye uwanja wa gofu wa Gymkhana, Arusha. Mashindano ya mwaka huu yamelenga kuuinua mchezo wa gofu Tanzania, kama sehemu ya mkakati wa NCBA wa kutunza mazingira.

Mashindano ya gofu ya NCBA yamethibitisha kuwa ni zaidi ya mashindano, kwa kuwaleta pamoja wachezaji, mashabiki, na wadau wa gofu, na kuzidisha ushirikiano kati ya benki ya NCBA na wateja wake.

Kama sehemu ya maandalizi ya tukio hilo, Benki ya NCBA iliandaa hafla ya upandaji miti siku ya tarehe 28, mwezi Juni 2024 katika hospitali ya jiji, Arusha, ambapo miti 1,000 ilipandwa, ikiwemo miti ya kivuli 700, na miti ya matunda 300. Juhudi hizi ni sehemu ya mkakati wa utunzaji mazingira wa NCBA kwa mwaka 2024; ambao umelenga kufanikisha upandaji wa miti 6,000 nchini Tanzania, sawasawa na dhamira ya serikali katika kutunza mazingira.


Claver Serumaga, Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano huo katika dhamira moja. “Kupitia ushirikiano wa mpango wetu wa gofu pamoja na juhudi za upandaji miti, tunaonyesha kujitolea kwetu kwenye mipango ya serikali katika utunzaji wa mazingira”. aliendelea kwa kusema “Jambo hili linaendana na mpango wa kampuni yetu mama katika kukuza mchezo wa gofu ndani ya Afrika mashariki, kuhamasisha mambo mazuri kwenye jamii, na kutoa jukwaa kwa wachezaji wakubwa wa gofu, na wale wanaochipukia”.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, mheshimiwa Damas Ndumbaro, ambaye alihudhuria tukio hilo kama mgeni rasmi, na pia alishiriki katika mchezo wa gofu, aliongelea ushirikiano wake kwa kusema; “ Serikali imefurahishwa kuona Benki ya NCBA ikichukua jukumu la msingi katika kuuinua mchezo wa golfu Tanzania. Mpango huu, ukijumlisha na upandaji wa miti, sio tu unakuza mchezo wa gofu peke yake, lakini inachangia katika juhudi za utunzaji wa mazingira, ikionyesha kuwa michezo inaweza kuleta mabadiliko chanya”.

KOBE MOTOR JAPAN KUONGEZA IDADI YA MAGARI YAKE SOKO LA TANZANIA

Mkuu wa Masoko (Head of Marketing) wa kampuni ya Kobe Motor ya Japan inayojishughulisha na uuzaji wa magari yaliyotumika kutoka Japan, Ken Aoki, akizungumza na mteja aliyefika katika banda la kampuni hiyo katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Kampuni hiyo imeanzisha utaratibu (leasing) ambapo mteja anaweza kulipa 35% ya gharama na kujipatia gari kutoka Japan huku kiasi kilichobaki akikilipa kwa miezi 12 hadi 24.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Kobe Motor inayouza magari yaliyotumika kutoka Japan, Victoria Ngomale (kulia akiwasikiliza wateja waliotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Kampuni hiyo imeanzisha utaratibu (leasing) ambapo mteja anaweza kulipa 35% ya gharama na kujipatia gari kutoka Japan huku kiasi kilichobaki akikilipa kwa miezi 12 hadi 24.
Mkuu wa Masoko (Head of Marketing) wa kampuni ya Kobe Motor ya Japan inayojishughulisha na uuzaji wa magari yaliyotumika kutoka Japan, Ken Aoki, akimsikiliza mteja aliyetembelea banda la kampouni hiyo katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Kobe Motor inayouza magari yaliyotumika kutoka Japan, Victoria Ngomale (kushoto) akimwelekeza jambo mteja aliyetembelea banda la kampouni hiyo katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Kampuni ya Kobe Motor ya Japan imesema itaendelea kujitanua zaidi katika soko la Tanzania kutokana na kukua kwa mahitaji ya magari ya aina mbali mbali kwa ajili ya mtumizi binafsi na ya kibiashara.

Ikiwa ni moja kati ya makampuni makubwa ya Kijapani yanayouza magari yaliyotumika kutoka Japan sehemu mbali mbali duniani, Kobe Motor tayari imeshauza zaidi ya magari 150,000 hapa Tanzania na sasa inalenga kuongeza uuzaji wa magari zaidi hapa Tanzania na eneo zima la Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kobe Motor Umar Ali, Tanzania ni moja kati ya nchi 10 zinazoongoza kwa soko la magari kutoka Japan ana kusema kuwa kampuni yake inaiona Tanzania kama soko muhimu.

“Lengo letu ni kuongeza uwepo wetu kwenye soko linalokuwa kwa kasi la Tanzania ambalo ni kitovu kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki,” alisema wakati akiongea na waandishi wa habari.

Akiongea kuhusu kampuni hiyo kuwa karibu na wateja wake alisema Kobe Motor inashiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam na kuwataka watu kutembelea banda la kampuni hiyo kwa ajili ya kupata ofa pamoja na kujishindia gari kutoka Japan kupitia bahati nasibu itakayoendeshwa viwanjani hapo.

Katika hatua nyingine, afisa mtendaji mkuu huyo alisema Kampuni ya Kobe Motor imezindua utaratibu wa wateja kulipa 35% ya thamani ya gari na kupewa gari la ndoto yao huku kiasi kilichobaki kikilipwa kwa kipindi cha miezi 12 au 24.

US GOVERNMENT & MINISTRY OF HEALTH UNITE TO PROMOTE HEALTH THROUGH NDONDO CUP 2024



Enthusiastic football fans from diverse corners of Dar es Salaam closely followed the launch Ndondo Cup 2024. The United States Government, in partnership with the Ministry of Health and the President’s Office - Regional Administration and Local Government (PORALG) in Tanzania, have partnered with the Ndondo Cup 2024 tournament to advance HIV and immunization services, an implementation which will be carried through the SITETEREKI youth platform, FURAHA YANGU men's Campaign, and CHANJO ni MAISHA Campaign, targeting eight regions in Tanzania, specifically Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Pwani and Kagera.
Evangelina Chihoma, who is a Strategic Information Specialist from PEPFAR addresses football fans in Dar es Salaam during the launch of Ndondo Cup 2024. 

Dar es Salaam, June 30th, 2024 - The Ministry of Health (MOH) has joined forces with the President's Office - Regional Administration and Local Government (PO-RALG), the United States Government (USG) - USAID and PEPFAR, through the Breakthrough ACTION project, the Ndondo Cup organizing committee, and sponsors CRDB and ASAS, to revolutionize healthcare in Tanzania through the power of football. The initiatives will be rolled out through the SITETEREKI youth platform, FURAHA YANGU men's campaign, and CHANJO ni MAISHA campaign, targeting eight regions in Tanzania, including Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Pwani and Kagera.

The tournament kicked off on June 30th, 2024, with an electrifying inaugural match between Manzese Warriors and Makuburi FC at the Kinesi Grounds in Sinza ward. Attendees had access to comprehensive health services, including HIV testing and treatment services, as well as vaccination services. Impressed by this innovative initiative, the Guest of Honor praised the organizing committee and sponsors for its forward-thinking approach, combining entertainment with health services.

"We are committed to pioneering innovative approaches that deliver tangible health outcomes," said Evangelina Chihoma from the PEPFAR Office. "We believe that sports can be a potent force for promoting behavior change and improving access to services, and we are thrilled to partner with the Ndondo Cup and Government of Tanzania to bring this initiative to life.”

MSIMU WA PILI WA MASHINDANO YA GOFU YA NCBA WAZINDULIWA NA UPANDAJI MITI ARUSHA

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na Claver Serumaga Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania wakiwa katika hafla ya kugawa zawadi kwenye uzinduzi wa mashindano ya NCBA Golf Series.

Arusha, Tanzania - Juni 29, 2024: Benki ya NCBA Tanzania imezindua rasmi msimu wa pili wa mashindano ya gofu ya NCBA. Mashindano haya yatafanyika kwenye uwanja wa gofu wa Gymkhana, Arusha. Mashindano ya mwaka huu yamelenga kuuinua mchezo wa gofu Tanzania, kama sehemu ya mkakati wa NCBA wa kutunza mazingira.

Mashindano ya gofu ya NCBA yamethibitisha kuwa ni zaidi ya mashindano, kwa kuwaleta pamoja wachezaji, mashabiki, na wadau wa gofu, na kuzidisha ushirikiano kati ya benki ya NCBA na wateja wake.

Kama sehemu ya maandalizi ya tukio hilo, Benki ya NCBA iliandaa hafla ya upandaji miti siku ya tarehe 28, mwezi Juni 2024 katika hospitali ya jiji, Arusha, ambapo miti 1,000 ilipandwa, ikiwemo miti ya kivuli 700, na miti ya matunda 300. Juhudi hizi ni sehemu ya mkakati wa utunzaji mazingira wa NCBA kwa mwaka 2024; ambao umelenga kufanikisha upandaji wa miti 6,000 nchini Tanzania, sawasawa na dhamira ya serikali katika kutunza mazingira.

Claver Serumaga, Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano huo katika dhamira moja. “Kupitia ushirikiano wa mpango wetu wa gofu pamoja na juhudi za upandaji miti, tunaonyesha kujitolea kwetu kwenye mipango ya serikali katika utunzaji wa mazingira”. aliendelea kwa kusema “Jambo hili linaendana na mpango wa kampuni yetu mama katika kukuza mchezo wa gofu ndani ya Afrika mashariki, kuhamasisha mambo mazuri kwenye jamii, na kutoa jukwaa kwa wachezaji wakubwa wa gofu , na wale wanaochipukia”.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, mheshimiwa Damas Ndumbaro, ambaye alihudhuria tukio hilo kama mgeni rasmi, na pia alishiriki katika mchezo wa gofu, aliongelea ushirikiano wake kwa kusema; “ Serikali imefurahishwa kuona Benki ya NCBA ikichukua jukumu la msingi katika kuuinua mchezo wa golfu Tanzania. Mpango huu, ukijumlisha na upandaji wa miti, sio tu unakuza mchezo wa gofu peke yake, lakini inachangia katika juhudi za utunzaji wa mazingira, ikionyesha kuwa michezo inaweza kuleta mabadiliko chanya”.

NSSF YATOA ELIMU KWA WATUMISHI WANAOTARAJIA KUSTAAFU

Mrisho Mwisimba - Meneja NSSF Ilala.

Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii NSSF umewataka watumishi wanaotarajiwa kustaafu kuanza kujiandaa ikiwa ni pamoja na kuhakiki taarifa zao za msingi sambamba na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha hali itakayosaidia kupunguza changamoto za maisha pindi wanapostaafu

Rai hiyo imetolewa na meneja wa mafao wa NSSF Ilala wakati akimuwakilisha mkurugenzi wa uendeshaji NSSF Mrisho Mwisimba wakati wa warsha iliyolenga kutoa elimu kwa watumishi wanaotarajia kustaafu kutoka katika mkoa wa Temeke ambapo pia amewasisitiza kuanzisha miradi salama ya uwekezaji ili kuwa na uhakika wa kipato endelevu.

Emmanuel Nyange, Meneja Idara ya Biashara wa Benki ya Biashra ya Taifa (TCB).

Kwa upande wake Emmanuel Nyange meneja idara ya biashara wa benki ya biashra ya taifa TCB , ambao pia walihudhuria mafunzo hayo kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha katika mafao amesema kuwa ,tcb imeamua kusimama na wastaafu kwa miaka 10 sasa ikijikita katika kutatua changamoto wanazokutana nazo wastaafu kwa kuanzisha akaunti maalumu ya Kivulini isiyo na makato yeyote wala gharama za uendeshaji,lengo likiwa ni kumnusuru mstaafu.

Nyange ameongeza kuwa Sambamba na hayo tcb imeanzisha huduma za pesheni advance inayomuwezesha mstaafu kupata fedha ya kujikimu kwa kutoa suluhu kwa tatizo analokutuna nalo,ila pia kuna huduma ya mkopo usio na masharti yeyote


Aidha kwa wastaafu watarajiwa tcb wanatoa huduma za fixed akaunti huku asilimia yake ikiwa ni mpaka asilimia 11 kwa mwaka, kupitia akaunti ya kivulini bado wastaafu wakipata majanga au ulemavu wa kudumu wanapewa fidia,na sababu kuu ni adhimio la serikali kuweza kufikia makundi yote katika huduma za ujumuishaji wa kifedha,

ITHUBA RECEIVES NATIONAL LOTTERY LICENSE IN TANZANIA


ITHUBA, Africa's leading National Lottery Operator, in collaboration with local partner SF Group, is thrilled to announce its expansion into Tanzania. The move was solidified by an official handover of a National Lottery license to ITHUBA Tanzania on the 28th June 2024 at a brief ceremony held at The Gaming Board of Tanzania headquarters in Dar es Salaam.

This marks a significant milestone in ITHUBA's commitment to driving social and economic development in the region. With an investment of $20 million, ITHUBA and SF Group are poised to revolutionize the Tanzanian lottery market with their innovative platform and exciting range of games.

The license handover was preceded by an official signing ceremony that took place on the 8th of May 2024, attended by members of ITHUBA and SF Group led by their Managing Director - an established businessman - Kelvin Koka. Also in attendance were members of the Board, Director-General, and the Management of the Gaming Board of Tanzania led by its Chairman, Ambassador Modest J. Mero.

Commenting on the recent events, Charmaine Mabuza, CEO of ITHUBA, shared her excitement: "We are delighted to join forces with SF Group to bring our technology and experience to the Tanzanian market to complement their expertise in the local market. Our platform, tailored specifically for this market, is equipped to deliver an unparalleled lottery experience to Tanzanian players. With new and exciting games on offer, we aim to capture the imagination of players and drive positive change in the community."

ITHUBA, along with SF Group, will soon begin the process of inviting retailers to sell and offer its products in Tanzania. Retailers stand to earn commissions and attract more footfall into their stores through the sale of lottery tickets.

TAFINA WATANGAZA UJIO WA KONGAMANO KUBWA LA UWEKEZAJI AFRIKA MASHARIKI (EAIF) 2024


Dar es Salaam, Tanzania - Julai 01, 2024 – Chama cha Fintech Tanzania (TAFINA) kinafuraha kutangaza Ujio wa Kongamano la Uwekezaji la Afrika Mashariki (EAIF) 2024, tukio la kihistoria ambalo litabadilisha hali ya teknolojia ya Afrika Mashariki. Kongamano hili, lililoandaliwa kwa ushirikiano na vyama vikuu vya fintech kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Tanzania, litafanyika Septemba 12 na 13, 2024, katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Tanzania.

EAIF 2024 ni tukio la siku mbili linalotayarishwa kuwa na mkusanyiko muhimu wa wadau wakuu katika sekta ya fintech. Inalenga kuchunguza na kujadili hali ya teknolojia ya kifedha inayobadilika na inayoendelea kwa kasi ndani ya Afrika Mashariki. Kwa kuzingatia uvumbuzi, uwekezaji na ushirikiano, kongamano hili linalenga kuwezesha mijadala muhimu , kuhimiza ushirikiano wa kimkakati, na kuvutia uwekezaji mkubwa katika eneo hili.

“Tunafuraha kubwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hili la Uwekezaji la Afrika Mashariki. Mada kuu ya kongamano hili ni " Invest & Partner : Leave No One Behind " Tunatumai kuwa kongamano hili litakuwa na mazungumzo ya maana na ushirikiano wa kimkakati, ubia na uwekezaji ndani ya mfumo ikolojia wa Fintech wa Afrika Mashariki,” alisema Cynthia Ponera, Mwenyekiti wa TAFINA.

Mwaka huu tupo na Selcom Tanzania, mdau wetu wa TAFINA ambaye ataratibu mfumo mzima wa malipo kuelekea kongamano hili ," aliongezea

Kwa upande wao Selcom

"Tunajivunia kuunganisha nguvu na TAFINA kwa ajili ya Jukwaa la Uwekezaji la Afrika Mashariki, tutatoa lango la malipo bila usumbufu kwa kila anayepanga kuhudhuria kongamano hili kupitia tovuti ya TAFINA – Shumbana Walwa, Mkuu wa Masoko wa Selcom Tanzania