Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 8 February 2022

MKURUGENZI WA VODACOM ATEMBELEA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NA KUJIONEA SHUGHULI MBALIMBALI

  • Apata fursa ya kujitambulisha kwa watoa huduma
  • Atoa tuzo na zawadi kwa wafanyakazi bora wa robo ya mwisho ya mwaka 2021
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose (kulia) akipata maelezo ya namna wateja wanavyohudumiwa kutoka kwa Meneja Uendeshaji wa kituo cha huduma kwa wateja Vodacom, Jombo Mkono wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea kituo hicho kilichopo mlimani city jijini Dar es Salaam ili kujitambulisha na pia kuona mambo mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia (kulia) na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Harriet Lwakatare (kushoto) wakati Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo alipotembelea kituo cha huduma kwa wateja kilichopo Mlimani city jijini Dar es Salaam na kutoa tuzo na zawadi kwa wafanyakazi bora wa robo ya mwisho ya mwaka 2021 na kuwaasa kuzingatia maadili na kutoa huduma bora zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose akizungumza na wafanyakazi wa kituo cha Huduma kwa Wateja Vodacom kilichopo Mlimani city jijini Dar es Salaam na kutoa tuzo na zawadi kwa wafanyakazi bora wa robo ya mwisho ya mwaka 2021 na kuwaasa kuzingatia maadili na kutoa huduma bora zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose akimkabidhi cheti Erick Mkunda kwa kutambua mchango wake katika kuhudumia wateja wa kampuni ya Vodacom.




No comments:

Post a Comment