Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 18 February 2022

DCB SKONGA YAENDELEA KUTOA FURSA KWA WATANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa DCB Skonga Klabu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto) akisalimiana na Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Alliance Life Insurance, Byford Mutimusakwa wakati wa uzinduzi wa DCB Skonga Klabu jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, Zacharia Kapama na Meneja wa Bima wa benki hiyo, Emanuel Kaganda.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama (wa pili kushoto) akisalimiana na Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Alliance Life Insurance, Byford Mutimusakwa wakati wa uzinduzi wa DCB Skonga Klabu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa na Meneja wa Bima wa benki hiyo, Emanuel Kaganda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kulia), Meneja wa Benki ya DCB Tawi la Mabibo, Al- Amin Lwano na Mkurugenzi Mtendaji wa Taste Tanzanite Catering Services, Vivian Kabipi wakifurahi wakati wa uzinduzi wa DCB Skonga Klabu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa DCB Skonga Klabu jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Ofisa Masoko wa DCB, Agness Ntabaye, Mkuu wa Wateja Binafsi, Fortunata Benedict na Ofisa Mahusiano, Bibiana Olomy.

Benki ya Biashara ya DCB imezindua Klabu maalumu kwa wateja wake wa akaunti maalumu ya elimu ya DCB Skonga iitwayo Skonga Klabu itakayokuwa na manufaa mbalimbali kwa wazazi, walezi pamoja na watoto.

Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa alisema jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Klabu hiyo kuwa hilo ni moja ya tukio lingine la kihistoria la Benki ya DCB na ni fursa kubwa katika jamii kipindi hiki benki yao ikitimiza miaka 20 tokea kuanzishwa kwake.

Alisema uzinduzi wa Skonga Klabu unaenda sambamba na mafanikio bora yaliyopatikana tokea wamezindua akaunti ya Skonga Septemba 10, 2019 akaunti iliyolenga kuleta suluhisho la uhakika wa elimu ya watoto hadi chuo kikuu.

“Benki imeweza kushuhudia mafanikio sambamba na kuboresha Maisha ya wateja wetu kwani akaunti hii inamuwezesha mteja wetu kuweka akiba kila mwezi kwa kipindi alichojiwekea kuanzia miaka mitatu na kuendelea, Mafanikio mengine ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya wateja wa skonga kufikia 3000 pamoja na ongezeko la amana kupitia akaunti hii ya akiba Zaidi ya Bilioni 1.

“Kupitia DCB Skonga akaunti imezaliwa DCB Skonga klabu, lengo la kuanzisha klabu hii ni Pamoja na kuongeza thamani kwa wateja wetu. klabu hii imesheheni faida lukuki, ni klabu ya aina yake tunayoianzisha kwa manufaa ya wote kuanzia wazazi, walezi pamoja na watoto, ni matumaini yangu wazazi watachangamkia fursa hii kujiunga na akaunti ya DCB Skonga ili kunufaika na faida za klabu hii”, alisema Bwana Ndalahwa.

Mzazi anachotakiwa kufanya ili kujiunga na Skonga Klabu mkurugenzi huyo alisema ni kufungua akaunti ya DCB Skonga na kuanza kuweka mpango wake wa kiasi cha kuanzia shs 100,000 ama zaidi kwa mwezi kwa ajili ya elimu ya mtoto na hapo anapata uanachama wa bure wa kujiunga na Skonga Klabu.

Akizitaja baadhi ya faida za klabu hiyo Bwana Ndalahwa alisema ni mzazi ama mlezi kupata kadi ya Visa credit card, kupata mkopo wa ada, kupata mkopo wa dharura wa hadi asilimia 90 ya amana yake, elimu ya masuala ya kifedha kwa watoto, huduma za ushauri kwa watoto, kujiunga na mpango maalumu kuhusiana na masuala ya akiba na uwekezaji Pamoja na michezo ya aina mbali mbali.

Aidha alisema wanachama wa skonga Klabu pia watahudhuria matukio mbalimbali ikiwemo kubadilishana mawazo na kushiriki programu mbalimbali za masuala ya uongozi, kuweza kupata punguzo mbalimbali za bei katika washirika wa biashara walioingia makubaliano nao mfano mahoteli, sehemu za michezo ya watoto, mbuga za Wanyama n.k.

“DCB Skonga Klabu imesheheni kila aina ya faida za kiuchumi, kielimu na burudani kwa wazazi na watoto, kwani kwa kupitia klabu hii watoto watapata taarifa za shule mbalimbali, maonyesho ya ajira, kupata nafasi ya kujiunga na programu ya kuwachukua wanafunzi wahitimu wa vyuo vikuu kujiunga na DCB lakini kama haitoshi wataweza kuhudhuria mafunzo ya ujasiriamali yatakayokuwa yakitolewa na asasi ya benki yetu.

“Skonga Klabu ni mahali pa kufanya marafiki wapya na kutengeneza kumbukumbu katika michezo, elimu ya masuala ya kifedha, stadi za kazi huku tukiwasaidia katika kutambua vipaji vya watoto na ili kufanya Skonga Klabu kuwa kivutio kwa watoto wetu wa rika tofauti, Benki ya DCB imewapanga katika mafungu manne ambapo watashiriki katika shughuli mbalimbali za michezo, mafunzo na vipaji kulingana na umri wao.

Bwana Ndalahwa aliongeza kuwa kwa kupitia DCB Skonga mzazi anaamua kiwango cha kuwekeza kila mwezi kwa ajili ya kutimiza ndoto zake lakini pia kupata uhakika wa elimu ya mtoto wake kwani endapo kutatokea majanga yatakayosababisha ulemavu wa kudumu ama kifo kabla ya muda kukamilika, mtegemezi atarudishiwa kiasi cha pesa kilichowekezwa tokea mwanzo na mtoto atalipiwa gharama zote za elimu pamoja na hela ya matumizi ya shule kwa kipindi chote kilichosalia cha mkataba.

Alisema kawa kupitia bidhaa hii ya DCB Skonga mteja anakuwa na uhakika wa usalama wa pesa zake, uhakika wa elimu ya mtoto hadi chuo kikuu, gawio nono la kila mwaka, uhakika wa mkopo wa dharura hadi asilimia 90 ya kiwango cha akiba alichowekeza, bima ya mazishi endapo mwenye akaunti/mume/mke au mtoto atakapofariki.

“Natoa wito kwa wazazi na watanzania wote kuchangamkia fursa zilizomo kwa kujiunga na akaunti ya DCB Skonga kwani kama tujuavyo kuwa fursa nyingine pia ya kuwekeza katika akaunti hii ni kupata gawio na hii tumeshafanya kwa wattage wetu wale waliokidhi vigezo waliweza kupata magawio yao katika mwezi uliopita wa Januari.

“DCB tumeweka kipaumbele katika kutekeleza mipango ya serikali ya awamu ya sita kwa kuleta bidhaa zinazochochea ufanisi wa sekta ya elimu nchini na pia katika kuhakikisha huduma zetu bora za kibenki zinawafikia watanzania wote nchini na katika kutoa fursa na bidhaa zenye tija kwa wateja wetu, elimu bora kwa kila mtanzania ni jambo muhimu sana sisi kama DCB ni matumaini yetu kuwa watanzania wataendelea kutumia fursa zinazopatikana katika akaunti ya DCB Skonga ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao.

No comments:

Post a Comment