Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 17 January 2020

“BENKI YA I&M YAANZA MAADHIMISHO YA KUTIMIZA MIAKA 10 KWA KURUDISHA KWA JAMII YA ARUSHA ”

I&M Bank Tanzania CEO, Mr. Baseer Mohammed explaining about the Bank’s donation to the Minister of Education, Science, Technology and Vocational Training, Hon. Professor Joyce Ndalichako.
Minister of Education, Science, Technology and Vocational Training, Hon. Professor Joyce Ndalichako and Regional Commissioner of Arusha, Hon. Mrisho Gambo in smiles after receiving 100 desks and chairs from I&M Bank Tanzania.
Minister of Education, Science, Technology and Vocational Training, Hon. Professor Joyce Ndalichako and Regional Commissioner of Arusha, Hon. Mrisho Gambo in a group photo with representatives from I&M Bank and other regional leaders.
I&M Bank officials led by the Bank’s CEO Mr. Baseer Mohammed in a group photo with the students of Mrisho Gambo Secondary School.
A snapshot of desks and chairs donated by I&M Bank to the Mrisho Gambo Secondary School in Arusha.
Arusha, Tanzania – Benki ya I&M kupitia sera yake ya kurudisha kwa jamii “Corporate Social Responsibility” imetoa msaada wa meza na viti 100 ili kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule ya sekondari ya Mrisho Gambo iliyopo jijini Arusha. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivo mbele ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mh.Joyce Ndalichako, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M Tanzania, Bw. Baseer Mohammed amesema Benki ya I&M inaitazama nchi ya Tanzania kiupekee katika kuchangia uchumi wa nchi za Afrika ya Mashariki na hivo wajibu wa Benki ya I&M kama sehemu ya jamii ya Tanzania ni kuhakikisha inachangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia utoaji wa huduma za kibenki kwa wateja wa reja reja, wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa.

“Kwetu Benki ya I&M hatuishii tu katika kuhakikisha tunatoa huduma bora za kibenki bali tumejiwekea utamaduni wa kuwekeza katika jamii ya Tanzania kama sehemu ya sera yetu ya kurudisha kwa jamii yaani Corporate Social Responsibility na hivo ushiriki wetu katika kuchangia shule hii ni ushahidi tosha wa dhamira yetu ya kuhakikisha tunachangia katika maendeleo ya jamii ya Tanzania”alisema Bw. Baseer.

Pamoja na msaada huo, Benki ya I&M kupitia kwa Afisa Mtendaji wake Mkuu Bw. Baseer Mohammed imeahidi kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii hususan mwaka huu ambapo Benki ya I&M inatimiza miaka 10 tangu kuingia nchini baada ya kuinunua iliyokua ikijulikana kama Benki ya CF Union mnamo mwaka 2010.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Proffesa Joyce Ndalichako ameishukuru Benki ya I&M kwa msaada huo ambao utachangia uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia wanafunzi wa shule hiyo na hivo kuunga mkono serikali katika jitihada zake za kuboresha sekta ya elimu.

Kuhusu Benki ya I&M
Benki ya I&M iliingia nchini Tanzania mwaka 2010 baada ya kuinunua iliyokua ikijulikana kama Benki ya CF Union ambayo ilianzishwa mwaka 2001. Katika kipindi cha miaka 10 tangu kuingia nchini, Benki ya I&M imeendelea kukua zaidi na kuweza kufungua matawi mapya 6 kutoka matawi mawili yaliyokua chini ya CF Union na hivyo kufikia jumla ya matawi 8. Matawi ya Benki ya I&M yanapatikana Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Benki ya I&M ni miongoni mwa Benki kongwe zaidi ikiwa imeanzishwa nchini Kenya mnamo mwaka 1974 na kusajiliwa katika soko la hisa la jijini Nairobi. Kwa sasa Benki ya I&M ina matawi katika nchi za Kenya, Rwanda, Tanzania na Mauritius.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Emmanuel Kiondo
Meneja Masoko na Mawasiliano
Benki ya I&M Tanzania
+255 743 858051/+255 683 365014
Emmanuel.Kiondo@imbank.co.tz

No comments:

Post a Comment