Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 3 December 2019

BENKI YA NBC NA T-PESA ZAINGIA USHIRIKIANO KUTOA HUDUMA ZA KIFEDHA

Mkurugenzi wa Huduma ya T-Pesa, Lulu Mkudde (kulia), akionyesha jinsi ya kufanya muamala wa kifedha kutoka katika akaunti ya Benki ya NBC kupitia huduma ya kifedha kupitia T-Pesa ya Kampuni ya TTCL, katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa huduma za kifedha kati ya T-Pesa na NBC ambapo wateja wa NBC wataweza kutoa na kutuma pesa kutoka katika akaunti zao kupitia huduma ya simu za mkononi ya T-Pesa. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Kibenki Kidigitali wa NBC, Deogratius Mosha. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Huduma za Kibenki Kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa huduma za kifedha kati ya NBC na T-Pesa ambapo wateja wa NBC wataweza kutoa na kutuma pesa kutoka katika akaunti zao kupitia huduma ya simu za mkononi ya T-Pesa. Kulia ni Mkurugenzi wa T-Pesa, Lulu Mkudde.
Mkurugenzi wa T-Pesa, Lulu Mkudde (kulia), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa huduma za kifedha kati ya NBC na T-Pesa ambapo wateja wa NBC wataweza kutoa na kutuma pesa kutoka katika akaunti zao kupitia huduma ya simu za mkononi ya T-Pesa. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Kibenki Kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha.
Mkurugenzi wa T-Pesa, Lulu Mkudde (kulia), akizungumza na maofisa wa NBC na wa T-Pesa mara baada ya uzinduzi wa ushirikiano wa huduma za kifedha kati ya NBC na T-Pesa ambapo wateja wa NBC wataweza kutoa na kutuma pesa kutoka akaunti zao kupitia huduma ya simu za mkononi ya T-Pesa. Kutoka kushoto ni; Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo, Mkuu wa Huduma za Kibenki Kidigitali wa NBC, Deogratius Mosha na Meneja Uendeshaji wa T-Pesa, Nasra Mughairy.

No comments:

Post a Comment