Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 18 December 2018

BENKI YA CBA NA VODACOM WAKABIDHI ZAWADI ZA BAJAJI MPYA TANO (5) KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA SHINDA NA M-PAWA

Mkurugenzi Idara ya Wateja Binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika (CBA), Julius Konyani (kushoto), akimkabidhi Mshindi wa Bajaji katika promosheni ya Shinda na M-PAWA,  Bi. Mariam Balawa mkazi wa Kibamba jijini Dar es Salaam, ambapo washindi watano walikabidhiwa bajaji zao na Bi Sophia mkazi wa Bukoba amekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni kumi. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika kwenye viwanja vya Benki hiyo Kijitonyama.  Anayeshuhudia (kulia) ni Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya.
Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla yakuwakabidhi washindi wa Bajaji katika promosheni ya Shinda na M-PAWA ambapo washindi watano walikabidhiwa bajaji zao na Bi Sophia mkazi wa Bukoba amekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni kumi. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika kwenye viwanja vya Benki hiyo Kijitonyama. Katikati ni Mkurugenzi Idara ya Wateja Binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika (CBA), Julius Konyani na kulia ni Meneja Biashara Huduma ya M-PAWA, Gloria Njiu.
Mkurugenzi Idara ya Wateja Binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika (CBA) Julius Konyani (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla yakuwakabidhi washindi wa Bajaji katika promosheni ya Shinda na M-PAWA ambapo washindi watano walikabidhiwa bajaji zao na Bi Sophia mkazi wa Bukoba amekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni kumi. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika kwenye viwanja vya Benki hiyo Kijitonyama, (kushoto) ni Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya na kulia ni Meneja Biashara Huduma ya M-PAWA, Gloria Njiu.

No comments:

Post a Comment