Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 14 November 2018

VODACOM FOUNDATION YADHAMINI PROGRAMU YA 'KUWA MJANJA' YA PSI

Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (watatu kushoto) akionyeshwa na Meneja miradi wa PSI Tanzania, Dkt. Anna Temba (wa pili kulia) ujumbe maalumu kwenye Tablet ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia elimu ya Afya kwa vijana wakati wa tamasha la Kuwa Mjanja lililofanyika katika shule ya Sekondari Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo ni maalumu kwa ajili ya vijana kupata elimu ya Afya lililoandaliwa na PSI kwa Udhamini wa Vodacom Tanzania Foundation. Kutoka kushoto ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Goba Magreth Richard, Agnes John, Mhamasishaji wa Vijana PSI Semeni Likulo na Pendo Raphael (kulia).
Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald (katikati ) akiwa pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam, wakielekezwa na mtaalam wa ubunifu wa kazi za mikono Flora Richard jinsi ya kutengeneza bangiri za batiki wakati wa Tamasha la Kuwa Mjanja ambalo ni maalumu kwa ajili ya vijana kupata elimu ya Afya iliyoandaliwa na PSI kwa Udhamini wa Vodacom Tanzania Foundation.
Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya sekondari Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam, wakijifunza elimu ya ujasiriamali wa kazi za mikono pamoja na Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald ( Kulia) wakati wa tamasha la Kuwa Mjanja ambalo ni maalumu kwa ajili ya vijana kupata elimu ya Afya, elimu ya ujasiriamali iliyoandaliwa na PSI kwa Udhamini wa Vodacom Tanzania Foundation. Tamasha hilo lilifanyika katika Viwanja vya shule ya msingi Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment