Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga (kulia) akipokea moja ya stika zilitolewa na Benki ya Posta kutoka kwa Meneja Masoko na Uendeshaji wa benki hiyo, Deo Kwiyukwa. (Kushoto) ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano Timotheo Mwakifulefule.
Leo Alhamisi, tarehe 6 Oktoba 2016. BENKI ya Posta Nchini (TPB) imetoa msaada wa stika zaidi ya 2,000 zenye namba za Wakuu wa Usalama Barabarani wa Mikoa yote nchini zitakazobandikwa kwenye mabasi yaendayo mikoani. Huu ni mwaka wa nne mfululizo benki hiyo anatoa stika hizo kwa lengo la kupunguza ajali katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka.
Leo Alhamisi, tarehe 6 Oktoba 2016. BENKI ya Posta Nchini (TPB) imetoa msaada wa stika zaidi ya 2,000 zenye namba za Wakuu wa Usalama Barabarani wa Mikoa yote nchini zitakazobandikwa kwenye mabasi yaendayo mikoani. Huu ni mwaka wa nne mfululizo benki hiyo anatoa stika hizo kwa lengo la kupunguza ajali katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka.
Akizungumza wakati wa kubandika stika walizozipokea katika mabasi hayo,
Kamanda Mkuu wa Usalama Barabarani Mohammed Mpinga, aliwataka madereva
kuendelea kuzingatia Sheria na kanuni za usalama barabarani ili kutokomeza
ajali zinazoendelea kupoteza maisha ya watu wengi. Alisema ofisi yake ilikuwa
inapokea maombi mengi kutoka kwa wananchi ili kupata namba zitakazowawesha
kutoa taarifa za madereva wanaofanya makosa wakiwa safarini.
Alisema kuwa stika hizo zitabandikwa katika mabasi yote yaendayo
mikoani pamoja na yae madogo maarufu kama Coastal.
"Tunaishukuru benki ya Posta kwa msaada huu kwani wametupa muda muafaka wa
kuelekea mwishoni mwa mwaka ambapo kumekuwa na ajali nyingi sana zinazopoteza
maisha ya watu wengi na kuwaacha wengine na ulemavu wa kudumu", alisema
Kamanda Mpinga.
Aliongeza kuwa Kitengo chake kitaendelea kushirikiana na TPB na wadau
wengine kuhakikisha wanaendesha kampeni hii na kutokomeza kabisa ajali za
barabarani.
Akikabidhi msaada huo Meneja Masoko na Uendeshaji wa TPB, Deo Kwiyukwa
alisema kuwa lengo la kutoa stika hizo ni kupunguza ajali na kupoteza nguvu
kazi ya Taifa katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka. Alisema kwa
kipindi cha miaka minne iliyopita toka waanze kampeni hiyo ajali nimeweza
kupungua kwa kiasi kikubwa kutokana na madereva kuhofia kuripototiwa na abiria
katika vyombo vya Usalama ambapo itapelekea kusimamishwa, faini kali au kifungo.
Deo aliwataka abiria kutumia vema namba hizo za simu kwa lengo la kudhibiti
mwendo mkali na kutokomeza kabisa ajali hizo. "TPB tunapenda kuwaasa
watumiaji wa mabasi ambao wengi ni wateja wetu kutoa taarifa katika vyombo vya
Usalama pale madereva wanaofanya makosa hasa.
Naye Afisa elimu kutoka Chama cha Kutetea Abiria (CHAKUA), Gervas
Rutagunziga alisema kuwa viashiria vya ajari ni vingi sana lakini wananchi hawapo
katika sehemu sahihi ya kulisemea jambo hilo, hivyo basi TPB inawapa nafasi kwa
abiria kuokoa maisha yao kwa kupiga simu pale ambapo wanakuwa hawaridhishwi na
mwendo kasi wa dereva au hali ya dereva kama amelewa au hajalewa.
"Mara nyingi abiria wamekuwa na uwezo wa kuzuia ajali lakini wanashindwa
kufanya hivyo kutokana na kutojua watafikisha vipi taarifa katika vyombo
husika, hivyo tunaamini kupitia stika hizi zenye namba za simu abiria sasa watakuwa
na uwezo mkubwa zaidi wa kulinda maisha yao" alisema Rutagunziga.
No comments:
Post a Comment