Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday 17 October 2015

KAMPUNI YA SIMU ZA TECNO YAZINDUA SIMU AINA YA PHANTOM 5 JIJINI DAR

Meneja Mauzo wa Simu za Tecno, Fred Kadilana akionesha simu aina ya Phanton 5 wakati wa uzinduzi wa tolea jipya la simu hizo uliofanyika Dar es Salaam hivi karibuni.
Wadau mbalimbli wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wadau mbalimbli wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Meneja Mauzo wa Simu za Tecno, Fred Kadilana (kulia), akitoa zawadi ya simu hiyo kwa baadhi ya waandishi waliouliza maswali mbalimbali juu ya ufanis wa toleo hilo.
Meneja Mauzo wa Simu za Tecno, Fred Kadilana (kulia), akitoa zawadi ya simu hiyo kwa baadhi ya waandishi waliouliza maswali mbalimbali juu ya ufanis wa toleo hilo.
Makampuni yanayozalisha Simu nchini yameshauriwa kuhakikisha wanakuwa wabunifu katika kusanifu na kulizasha simu bora ili kwenda sambamba na soko la dunia.

Wito huo umetolewa na Meneja mauzo wa simu za Tecno, Fred Kadilana wakati wa uzinduzi wa tolea jipya la simu ya Phantom 5 uliofanyika Dar es Salaam hivi karibuni.

Kadilana alisema soko la bidhaa zao linakuwa kwa kasi hususan barani Afrika hivyo wanafanya jitihada kuhakikisha wanakwenda sambamba na soko la dunia.

"Soko la dunia linakuwa kwa kasi na hata bidhaa zetu pia hivyo tunajitahidi kila kukicha kwenda sambamba na ukuaji wa mahitaji ya wananchi," alisema Kadilana.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa kampuni hiyo, Daniel Xu alisema falsafa ya kutengeneza simu bora ni kulenga mahitaji ya soko la dunia.

Alisema simu ya Phanthom 5 ni toleo linalowapa wateja usanifu wa kipekee wenye uwezo 32GB katika uhifadhi wa taarifa na pia 3 GB katika mfumo wa kusoma na kuperuzi katika simu kwa haraka zaidi.

"Simu hii ina uwezo wa 300m Ah katika betri lake hivyo kuondoa usumbufu wa kuchaji simu mara kwa mara," alisema Xu.

Xu alisema kutokana na changamoto za kidunia simu hiyo ina uwezo wa kufurahia mawasiliano katika mazingira mbalimbali.

Aliongeza kuwa kwa kuzingatia ubora Tecno imeweza kushinda tuzo ya dunia kwa ubora na kwa sasa wanaongoza kwa mauzo kwa kipindi cha miaka mitano sasa barani Afrika.

No comments:

Post a Comment