Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday, 28 March 2015

RAIS WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE AFUNGUA KONGAMANO LA VIJANA AFRIKA NA CHINA, RAIS JAKAYA KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA

Mgeni Rasmi wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China, Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe akihutubi usiku huu kweye kongamano hilo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza usiku huu kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha, ambapo Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China linafanyika na mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (aliyeshikwa mabega) akiwasili usiku huu kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha, kwa ajili ya kufungua Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China.
Rais Jakaya Kikwete akipewa tunzo ya Heshima ya juu ya Kuhamasisha Amani na Utulivu katika Bara la Afrika na Rais wa Umoja wa Vijana Afrika (PAYU), Francine Furaha Muyumba. Tuzo hiyo imetolewa na Umoja wa Vijana wa Umoja wa Afrika. Pichani kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Mboni Mhita.
Rais Jakaya Kikwete akitoa salamu zake kwa washiriki wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China, ambalo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya washiriki wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China, ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana .
Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipowasili jioni ya leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha, kwa ajili ya kutoa salamu kwa washiriki wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China, ambalo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe. Pichani kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Stephen Masele.

PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA.

No comments:

Post a Comment