Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 24 March 2015

DIAMOND MOTORS WAZINDUA GARI JIPYA LA MITSUBISHI 2015 ASX JIJINI DAR ES SALAAM

Wema Sepetu akiwasha gari Jipya la ASX Mitsubishi katika uzinduzi wa gari hilo jijini Dar es Salaam.
Hili ndilo gari la ASX Mitsubish jipya lililozinduliwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo na mwigizaji maarufu nchini, Wema Sepetu wamesifia gari jipya la Mitsubishi ASX la mwaka 2015 linalouzwa na kusambazwa na kampuni ya Diamond Motors (Hansa Group).

Katika uzinduzi wa kutambulisha gari hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine Kampuni ya Diamond Motors wauzaji pekee wa magari kutoka Mitsubishi waliwaalika Millard Ayo na Wema Sepetu kujaribu gari hilo toleo jipya Mitsubishi ASX kabla ya uzinduzi.

Mastaa hao walivutiwa na mwonekano wa Mitsubishi ASX lenye vioo vya kisasa juu vyenye mwanga unaomwezesha dereva na abiria kufurahia mwonekano wa pande zote.

Meneja mauzo wa Diamond Motors, Reena Ganatra alisema Gari hilo lenye luninga ndogo inayocheza DVD, iPods, Bluetooth na sauti kutoka vyanzo mbalimbali ni maalumu kwa vijana wa kisasa na familia kwani Mitsubish ASX limetengenezwa na teknolojia ya MIVEC yenye kulifanya liwe na nguvu ya 150 ps katika 6,000 rpm na nguvu ya kuzunguka kwa mwendokasi mkubwa na kwamba limetengenezwa maalum kutumia mafuta kidogo.

“ASX ni mwanzo tu, tunazo aina nyingine za magari kama Pajero ambayo tunakaribia kuyatambulisha sokoni ili kuwapatia watanzania magari imara na yenye kuaminika kutoka Mitsubishi” Alisema Ganatra.

ASX toleo la 2015 limebuniwa kwa ubora wa hali ya juu na imara likiwa na bodi gumu pia lina mfumo maalumu usiotegemea funguo hivyo kumfanya mwendeshaji kuwasha injini kwa kubofya kitufe.

“ASX kutoka Mitsubishi, imetengenezwa maalumu kukidhi mazingira ya Tanzania hasa mijini kama Dar es Salaam ambapo muda wowote dereva wa kawaida anatoka kwenye barabara nzuri na kuingia kwenye barabara zenye makorongo” alisema Ganatra

Injini ya gari hilo ambayo ni 2.0-liter imeunganishwa INVECS-III CVT inayoisaidia mwendelezo wake katika kubadili mwendo pamoja na uimara wa usukani unaosaidia mikono ya dereva kuwa salama hata anapokuwa katika mwendo mkali.

Hansa Group inayofanya biashara kama Diamond Motors Limited, imekuwa ikifanya kazi katika sekta ya usafirishaji tangu mwaka 1980, ikitoa huduma kwa wasambazaji na wadau wa usafiri. Kampuni hiyo huhusika na bidhaa / huduma mbalimabali. Shughuli za Hansa Group zimesambaa karibu nchi zote za jumuia ya Africa ikitoa huduma kama vile za uchimbaji, umeme, mafuta na gesi, reli, ulinzi, ujenzi, usafiri, kimataifa na jumuhia za kimataifa.

Dewji Blog

No comments:

Post a Comment