Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday 9 August 2014

WAZIRI WA UJENZI DK. MAGUFULI AIFAGILIA NSSF UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ameusifu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa daraja la Kigamboni.

Ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo mpaka sasa NSSF imetoa sh. bilioni 117 kati ya Bilioni 214 zitakazokamilisha ujenzi wa daraja hilo.


Akizungumza leo jijini Dar es salaam, alipotembelea daraja kuona namna ujenzi unavyoendelea, Dk. Magufuli alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo umekutana na changamoto nyingi ikiwemo kina kilichokuwa katikati ya bahari kupoteza malighafi ya ujenzi ambapo wahandisi waliamu kufanya utafiti.


Alisema kuwa juhudi za NSSF  katika kufadhili mradi huo umewezesha changamoto zilizokuwa zikiukabili maradi huo kufanyiwa kazi.


Naye Kaimu Mkurugenzi wa NSSF, Ludovick Mrosso, alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika Julai, 2015 ambapo katika daraja zitakuwa barabara sita za magari, mbili za wapita kwa miguu.Maradi huo unajengwa kwa kushirikisha Wizara ya Ujenzi, NSSF na Tanroads.



Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka kwa Meneja wa Mradi wa ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi Kareem Mataka, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo.

Mh. Magufuli akifafanua akitoa maelekezo kwa Mhandisi Kareem Mataka (kulia).

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni linalojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii  (NSSF), kwa kushirikiana na Serikali. Kulia ni  Meneja Mradi ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Kareem Mataka.

Waziri akiwa katika zira ya ukaguzi pamoja na maofisa kutoka Wizara ya Ujenzi, NSSF pamoja na waandishi wa habari.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ludovick Mrosso akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.

Bofya hapa kwa picha zaidi

Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment