Benki yaendelea kufungua fursa za mitaji, mafunzo na ushirikiano kupitia programu za Go Green na iMBEJU
Benki ya CRDB imeeleza dhamira yake ya kuongeza fursa za ufadhili kwa vijana wenye mawazo na miradi bunifu inayolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza uchumi wa kijani, kutengeneza ajira na kujenga ustahimilivu wa jamii dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.
Kupitia jitihada hizo, benki inalenga kuwawezesha vijana kupata mitaji, elimu na ushirikiano utakaowasaidia kubadili mawazo yao bunifu kuwa biashara endelevu na suluhisho zinazochangia utunzaji wa mazingira na maendeleo ya jamii.
Dhamira hiyo imeelezwa na Meneja wa Uhusiano wa Taasisi za Kimataifa wa Benki ya CRDB, Terence Mponjoli, wakati akishiriki mjadala kuhusu ufadhili wa biashara zinazoongozwa na vijana katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuzingatia haki na kuimarisha ustahimilivu wa jamii.
Mjadala huo ulifanyika pembezoni mwa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), unaofanyika jijini Antalya, nchini Türkiye.
Mponjoli amesema Benki ya CRDB inaendelea kuwekeza katika suluhisho za kifedha zinazochochea maendeleo endelevu, ikiwemo programu yenye thamani ya dola za Marekani milioni 200 inayolenga kuimarisha ustahimilivu wa sekta ya kilimo dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.
Ameeleza kuwa Benki ya CRDB, ikiwa taasisi pekee ya fedha nchini Tanzania yenye ithibati ya Mfuko wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Fund – GCF), ina nafasi muhimu katika kufungua fursa za ufadhili wa miradi inayochangia kukabiliana na changamoto za kimazingira.
Aidha, kupitia taasisi yake ya CRDB Bank Foundation pamoja na programu za Go Green na iMBEJU, benki hiyo inaendelea kuwawezesha vijana na wanawake kwa kuwapatia mitaji, mafunzo na fursa mbalimbali za kuanzisha na kukuza biashara zinazolinda mazingira na kuchochea uchumi wa kijani.

.jpeg)
.jpeg)



.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)






.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)





.jpeg)