Foreign Exchange Rates

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

CRDB Bank Advert_070325

Monday, 11 May 2026

NMB YAHIMIZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI DODOMA KURASIMISHA VIKUNDI VYAO ILI KUPATA FURSA ZA KIFEDHA

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango, akizungumza na wanawake wajasiriamali wakati wa hafla ya Siku ya Mama iliyofanyika jijini Dodoma, ambapo NMB ilitoa elimu ya fedha na kuhimiza urasimishaji wa vikundi ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo na huduma nyingine za kifedha.

Dodoma — NMB Bank Plc imewahimiza wanawake wajasiriamali nchini kurasimisha vikundi vyao ili waweze kutambulika kisheria na kunufaika zaidi na mikopo, elimu ya fedha pamoja na huduma nyingine za kifedha zinazolenga kukuza shughuli zao za kiuchumi.

Akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Mama iliyofanyika jijini Dodoma, Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango, alisema wanawake wengi wana uwezo mkubwa wa kufanya biashara na kuchangia maendeleo ya familia pamoja na taifa, lakini changamoto ya kutokuwa katika vikundi vilivyosajiliwa imekuwa ikiwanyima fursa ya kufikiwa kirahisi na taasisi za kifedha.

Alisema urasimishaji wa vikundi unaongeza uaminifu, nidhamu ya kifedha na uwezo wa wanawake kupata mikopo yenye masharti nafuu, elimu ya ujasiriamali, huduma za kidijitali pamoja na ushauri wa usimamizi wa fedha.

Wanawake wanapaswa kuona umuhimu wa kufanya kazi katika vikundi vilivyosajiliwa ili iwe rahisi kupata huduma rasmi za kifedha na kuongeza uwezo wa kukuza biashara zao,” alisema Shango.

Aidha, aliwahimiza wanawake kutumia mikopo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha wanarejesha kwa wakati ili kujenga historia nzuri ya kifedha ambayo itawasaidia kupata fursa zaidi za kifedha siku zijazo.

Kwa upande wake, mmoja wa wajasiriamali walioshiriki hafla hiyo, Sharifa Mohamed, alisema mikopo kutoka NMB imemsaidia kuongeza mtaji na kupanua biashara yake hatua kwa hatua.

Aliipongeza benki hiyo kwa kuendelea kutoa elimu pamoja na fursa kwa wanawake wajasiriamali, akisema hatua hiyo imekuwa chachu ya kuwafanya wanawake wengi kujitegemea kiuchumi na kuboresha maisha ya familia zao.

Hatua hiyo inaonesha dhamira ya NMB kuendelea kusaidia ukuaji wa wanawake wajasiriamali kupitia huduma za kifedha jumuishi, elimu ya fedha na uwezeshaji wa kiuchumi katika jamii mbalimbali nchini.





No comments:

Post a Comment