Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 29 December 2025

VODACOM KANDA YA ZIWA YAGUSA MAISHA YA WATEJA KUPITIA KAMPENI YA KUGAWA MAKAPU YA SIKUKUU

Kagera, 29 Desemba 2025 — Timu ya Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa imeendelea kuonesha mshikamano na kuthamini uaminifu wa wateja wake kwa kusambaza upendo kupitia zoezi la kugawa Makapu ya Vodacom, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea msimu wa sikukuu na kuhitimisha rasmi maadhimisho ya miaka 25 ya utendaji wa kampuni hiyo nchini Tanzania.

Hafla hiyo imefanyika katikati ya mwezi Desemba katika Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera, ambapo wateja mbalimbali walipatiwa makapu yenye mahitaji ya msingi kama ishara ya shukrani na kuthamini mchango wao katika safari ya mafanikio ya Vodacom Tanzania kwa kipindi cha robo karne.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, wawakilishi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa walisema kuwa kampeni hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa karibu kati ya kampuni na wateja wake, huku ikiendeleza utamaduni wa kushiriki furaha na jamii inayoiwezesha kampuni kukua na kuendelea kutoa huduma bora za mawasiliano.

Tunatambua kuwa mafanikio ya Vodacom Tanzania kwa kipindi cha miaka 25 yasingewezekana bila uaminifu na ushirikiano wa wateja wetu. Ndiyo maana tumeona ni muhimu kusherehekea msimu huu wa sikukuu pamoja nao na kuwashukuru kwa vitendo,” ilielezwa.

Wateja waliopokea makapu hayo walieleza kufurahishwa na hatua hiyo, wakisema kuwa inaonesha namna Vodacom inavyothamini wateja wake zaidi ya kutoa huduma za mawasiliano, bali pia kama mshirika wa kijamii anayeangalia ustawi wa jamii kwa ujumla.

Kupitia kampeni hii ya kugawa makapu, Vodacom Tanzania inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuwajibika kijamii, huku ikitumia maadhimisho ya miaka 25 kama fursa ya kuimarisha mshikamano, upendo na ushirikiano na wateja wake kote nchini.

No comments:

Post a Comment