Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Sunday, 21 September 2025

MKUU WA MKOA AZINDUA TAWI JIPYA LA EQUITY BANK GEITA

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela, amezindua rasmi tawi jipya la Benki ya Equity mjini Geita na kutoa wito kwa benki hiyo kuhakikisha inatoa mikopo kwa wanunuzi wa dhahabu ili kupunguza utegemezi wa mikopo kutoka nje ya nchi.

Fursa za Kifedha kwa Wananchi

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Shigela alisema huduma za kifedha zinazotolewa na Equity Bank zitakuwa chachu ya kukuza uchumi wa ndani kwa kuwasaidia wachimbaji wadogo, wakulima, wafanyabiashara na wajasiriamali kupata mikopo nafuu.

Alisisitiza kuwa mkoa wa Geita una nafasi kubwa ya kustawi kiuchumi iwapo sekta ya madini itawezeshwa ipasavyo kupitia huduma bora za kifedha.

Mkakati wa Kitaifa wa Equity

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania, Isabela Maganga, alisema kufunguliwa kwa tawi la Geita ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa benki hiyo kuhakikisha wananchi wanapata huduma karibu na maeneo yao, hususan katika mikoa yenye shughuli kubwa za kiuchumi.

Alibainisha kuwa Equity itaendelea kuwekeza kwenye sekta za kimkakati ikiwemo madini, kilimo na biashara ndogo na za kati.

Huduma kwa Wachimbaji na Wafanyabiashara

Naye Meneja wa tawi jipya la Geita, Hilary Mpaswa, aliahidi kuwa benki hiyo itakuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha wachimbaji na wafanyabiashara kupitia mikopo nafuu na huduma bora za kifedha.

Maoni ya Wafanyabiashara

Baadhi ya wafanyabiashara wa mjini Geita akiwemo Leonard Bugomola na Richard Eliniko walipongeza hatua hiyo, wakisema itakuza ushindani na kuboresha huduma za kibenki mkoani humo.




No comments:

Post a Comment