Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja iliyofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. |
Dar es Salaam: Oktoba 7, 2024: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua maadhimisho ya mwezi wa huduma wa kwa wateja huku ikijivunia mafanikio mbalimbali ikiwemo maboresho makubwa ya huduma zake yanayolenga kukidhi mahitaji ya wateja wa benki hiyo (Customer satisfaction).
“Zaidi tumefanya maboresho makubwa kwenye Mfumo wa ulipaji wa malipo ya serikali kupitia mfumo wa GEPG unaowapa wateja wetu uwezo wa kufanya malipo ya Serikali na kulipia ankara zao kwa urahisi zaidi.’’ Aliongeza huku akitumia fursa hiyo pia kutambulisha huduma mpya ya “Self Service Account Opening” inayotoa fursa kwa wateja wateja wa benki hiyo wanaotumia huduma za NBC Kiganjani na Tovuti ya NBC kuweza kufungua akaunti wao wenyewe popote walipo.
Akizungumzia maboresho kwenye utoaji wa mikopo ya benki hiyo, Sabi alitaja uwepo wa maboresho makubwa kwenye vigezo tofauti vinavyotumika katika utoaji wa mikopo mbalimbali ya benki hiyo ikiwemo Mikopo ya Wastaafu, mikopo inayochukuliwa kwa Dhamana ya Hatifungani (BOND), Mikopo ya Nyumba (Mortgage) na mikopo ya kilimo na ufugaji lengo likiwa ni kuwezesha ufikiaji wa wadau wengi zaidi wa sekta hizo ili waweze kunufaika na huduma za benki hiyo.
“Kwa mfano, mbali na mikopo ya wastaafu ambapo kwa sasa kiasi cha juu cha mkopo hiyo kimeongezeka kutoka Sh50 Milioni mpaka Sh300 Milioni pia tumeboresha vigezo vya upatikanaji wa mikopo ya nyumba yaani “Mortage” ambapo sasa mteja anaweza kukopa mpaka kiasi cha Sh. 1 Bilioni kwa muda wa miaka 25. Zaidi tumefanya uwezeshaji mkubwa katika sekta ya Kilimo ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania wote ambapo tumetoa mikopo ya matrekta, Bima kwa Wakulima na kuanzisha Akaunti maalumu kwa ajili ya wafugaji.’’ Alitaja.
Wakizungumza kwenye hafla hiyo baadhi ya wateja wa muda mrefu wa benki hiyo walionyesha kuridhishwa na mabadiliko ya kihuduma yanayoendelea kufanywa na benki hiyo huku wakionesha kuguswa zaidi na hatua ya benki kuendelea kuboresha mazingira ya utoaji wa mikopo mbalimbali kwa kuondoa vigezo ambavyo havikuwa rafiki kwa baadhi ya wananchi wakiwemo wastaafu na wale ambao hawapo katika sekta rasmi.
“Kwa sisi ambao tumehudumiwa na benki hii kwa zaidi ya miaka 30 sasa tumejionea mabadiliko makubwa yanayohusisha maboresho chanya ya huduma za benki ya NBC. Licha ya taasisi nyingi za fedha kutokuwa na vigezo rafiki katika utoaji wa mikopo kwa wastaafu ni faraja kwetu kuona kwamba NBC ndio kwanza wameongeza ukomo wa umri wa mkopaji kutoka Miaka70 mpaka Miaka 80’’
“Hatua hii faraja kwetu zaidi kwa kuwa ukomo wa miaka 70 uliokuwepo hapo awali ulikwamisha jitihada zetu za kujikwamua kiuchumi wakati ambao sisi binafsi tulihisi bado tuna nguvu na wajibu wa kuendesha shughuli zetu kiuchumi,’’ alisema Bw Francis Mfundo kauli ambayo iliungwa mkono na wateja wenzie, Asaa Simba pamoja nae Zuhura Maganga.
No comments:
Post a Comment