Aidha katika ziara hii Timu ya NBC ilipata nafasi ya kumsalimu Mhasibu Mkuu wa Serikali Ndg.Leonard Mkude katika Ofisi za Wizara ya Fedha Dodoma pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa TARURA Eng.Victor Seff katika Ofisi za TARURA zilizoko Mtumba Dodoma
Akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni, iliyoandaliwa na NBC katika viwanja vya Collina Hoteli ambayo ilihudhuriwa na baadhi ya wateja. Mkurugenzi wa wateja wakubwa NBC, Bw.James Meitaron, Amesema “Tunaamini kuwa ufunguo wa kuwa mtoa huduma wa kipekee ni kuelewa mahitaji na matakwa ya wateja wetu. Hivyo kupitia ziara hizi tunapata mapendekezo na ushauri wenye suluhu zenye ubunifu wa kuboresha uzoefu wa kibenki kwa ujumla”
Benki ya taifa ya biashara NBC wameahidi kuendelea kujali na kusikiliza matakwa ya wateja wao ambapo hivi karibuni wanatarajia kuendeleza ziara hiyo katika mkoa wa kanda ya ziwa ambao ni Mwanza pamoja na mkoa uliopo kanda ya kaskazini Arusha.
No comments:
Post a Comment