Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 23 May 2024

MKURUGENZI WA PBZ BANK ARAFAT HAJI AKUTANA NA TIMU YA UONGOZI


Mkurugenzi Muendeshaji wa PBZ Bank, Ndg. Arafat Ally Haji, amekutana na kufanya mazungumzo na timu yake ya uongozi wa PBZ Bank ikiwa ni siku yake ya kwanza kuingia ofisini baada uteuzi wake na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi. 


Mkurugenzi Arafat alikuwa ni Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Bima la Zanzibar kabla ya uteuzi huu, ambapo amekuwa akikabidhi majukumu, kabla kuingia rasmi kwenye majukumu mapya kama Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Bank). 


PBZ Bank ni Miongoni mwa mabenki makubwa Tanzania, ikiwa na Rasilimali za Trilioni 2.05, Amana Trilioni 1.73, na Faida kabla ya kodi ya Bilioni 75.2 kwa mujibu wa hesabu za Mwaka 2023, ikiiweka benki kwenye nafasi ya 7 miongoni mwa Mabenki 44 yaliopo Tanzania.

No comments:

Post a Comment