Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 5 April 2024

VODACOM YAKABIDHIWA CHETI CHA USAJILI ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Cheti cha Usajili wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC - Olaf Mumburi mara baada ya kuzindua tume hiyo jijini Dar es Salaam tarehe 3 Aprili 2024.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom wakiwa kwenye uzinduzi mara baada ya kukabidhiwa cheti cha usajili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alizindua Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na mifumo ya usajili na malalamiko ya ukiukwaji wa misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 3 Aprili 2024.

Tukio hili lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mawaziri, Mabalozi, pamoja na Wageni mbalimbali.

Makampuni, Mashirika, na Taasisi mbalimbali zimetunukiwa Cheti cha Usajili kwenye Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Moja ya Makampuni yaliyotunukiwa Cheti hicho ni Vodacom Tanzania. Hii ni baada ya kuwa kampuni ya mwanzo kusajili ulinzi wa taarifa binafsi za wateja wake hapa Tanzania.

No comments:

Post a Comment