Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 23 June 2023

WATEJA WA TOTALENERGIES KURUDISHIWA 10% KUPITIA USHIRIKIANO NA LIPA KWA M-PESA

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania PLC, Bi. Harriet Lwakatare (kushoto) na Meneja Masoko wa TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, Caroline Kakwezi (kulia) wakifurahia baada ya uzinduzi wa ushirikiano utakaowawezesha wateja wa TotalEnergies kulipa kwa LIPA kwa M-Pesa masaa 24, siku 7 za wiki kwenye vituo vyote vya kutolea huduma na maduka yote ya Bonjour nchini kote uliofanyika Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pia, wateja watarudishiwa 10% ya pesa watakapolipia kwa kutumia M-Pesa kwa siku 15 zijazo na kila Jumamosi kwa miezi mitatu ijayo.

Mteja wa TotalEnergies, Bw. Ambrose Kumbila (mwenye bodaboda) akifurahia pamoja na Meneja Masoko wa TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, Caroline Kakwezi (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania PLC, Bi. Harriet Lwakatare (wa pili kulia), na Meneja Uendeshaji wa Mtandao wa TotalEnergies, Bw. Thomas Meitaron (katikati), pamoja na Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa Sheria, Bw. Agapinus Tax (wa kwanza kushoto) mara baaya ya kulipia mafuta kwa kutumia LIPA kwa M-Pesa muda mfupi baada ya kuzinduliwa rasmi kwa huduma hiyo ikiwa ni ushirikiano baina ya huduma ya M-Pesa ya Vodacom na TotalEnergies kuwawezesha wateja wa TotalEnergies kufanya malipo kwa masaa 24, siku 7 za wiki kwenye vituo vyote vya kutolea huduma na maduka yote ya Bonjour nchini kote. Pia, wateja watarudishiwa 10% ya pesa watakapolipia kwa kutumia M-Pesa kwa siku 15 zijazo na kila Jumamosi kwa miezi mitatu ijayo.


Dar es Salaam - Juni 21, 2023: Kupitia dhamira ya kuendeleza mfumo wa maisha wa kutotumia pesa taslimu nchini, huduma ya M-Pesa ya Vodacom na TotalEnergies Marketing Tanzania Limited wamezindua ushirikiano wa kimkakati ili kuwawezesha wateja kufanya malipo bila ya kutumia pesa taslimu kwa usalama na urahisi katika vituo vyote vya kutolea huduma vya TotalEnergies.

Kupitia ushirikiano huu mpya, wateja watafurahia faida tofauti ikiwemo kurudishiwa 10% ya pesa watakapolipia kwa kutumia M-Pesa kwa siku 15 zijazo. Ofa hii itaendelea mbele zaidi kwa kila Jumamosi kwa miezi mitatu ijayo. Zaidi ya hapo, kupitia ushirikiano huu, pia wateja watapata huduma ya M-Pesa kwa shughuli za kibiashara ikiwamo kuweka, kutoa, na kutuma pesa wakiwa katika katika vituo vya kutolea huduma vya TotalEnergies.

Ushirikiano wa TotalEnergies na huduma ya M-Pesa ya Vodacom umekuja katika muda muafaka, sio kuwapa Watanzania njia rahisi na ya uhakika ya kutumia pesa bali pia kuunga mkono jitihada za kidigitali za serikali hususani kuchochea mabadiliko kuelekea kwenye uchumi wa kidigitali ambapo bado matumizi ya pesa taslimu yanaendelea kutumika na kukubalika maeneo mengi nchini kote.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huu uliofanyika katika kituo cha kutolea huduma cha TotalEnergies kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania PLC, Bi. Harriet Lwakatare amesisitiza namna ambavyo kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele kwenye kuunga mkono ajenda ya Tanzania ya kidigitali na kuwa ushirikiano huu mpya ni hatua mojawapo kuelekea njia sahihi.

“Tunaendelea kujikita katika kutoa ubunifu wa ufumbuzi wa kidigitali kuhakikisha tunasaidia mamilioni ya Watanzania kujiunga na kushiriki katika uchumi wa kidigitali. hili linathibitishwa kwa ubunifu tunaoendelea kuufanya katika kuunga mkono ajenda ya kutotumia pesa taslimu ambapo M-Pesa ina mchango muhimu ambapo tumeleta mapinduzi ya namna tunavyofanya malipo. Ushirikiano huu utasaidia wateja wa TotalEnergies kulipia kwa urahisi kupitia M-Pesa kwa kufuata hatua chache kwenye simu zao za mkononi na kupata huduma mbalimbali kwa urahisi na usalama wa miamala yao wakiwa katika vituo vya kutolea huduma vya TotalEnergies,” alisema Bi. Lwakatare.

Kwa upande wa TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, Meneja Masoko, Caroline Kakwezi ameelezea kuwa, “TotalEnergies imevutiwa na jitihada za Vodacom kuunga mkono kasi ya utekelezaji wa dhamira ya serikali ya kutumia mifumo ya kidigitali kwenye kuleta uchumi jumuishi Tanzania kupitia M-Pesa. Ushirikiano huu kati ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited na huduma ya M-Pesa ya Vodacom unaendelea kuchochea zaidi juhudi hizi kwa kuwawezesha wateja kulipia mafuta kupitia Lipa Kwa Simu na kupata huduma za M-Pesa za kuweka na kutoa pesa. Ushirikiano huu mpya unalenga kuwajengea hali ya kujiamini katika matumizi ya majukwaa ya kifedha ya kidigitali kwa kupunguza hatari na mzigo unaosababishwa na kutembea na pesa taslimu. Kwa pamoja, Vodacom na TotalEnergies tutaendelea kujizatiti kutoa huduma bora kwa wateja.”

Miaka 10 iliyopita na zaidi, Tanzania imeshuhudia mwamko mkubwa wa matumizi ya huduma za pesa kwa njia ya simu za mkononi kama vile M-Pesa ambayo inaoongoza njia kwa upande wa malipo ya kidigitali. ikiwa na wateja zaidi ya milioni 10 na wafanyabiashara zaidi ya 180,000 kwenye mtandao wake wakitoa huduma ya LIPA KWA M-Pesa na suluhisho kwa huduma za wafanyabiashara, M-Pesa inaendelea kuwa kinara kupitia ubunifu wa ufumbuzi wa malipo ya kidigitali ambayo yanaleta urahisi, ufanisi na hatimaye kuchochea ujumuishi wa huduma za kifedha kwa Watanzania wote.

Kwa kuongezea, kampuni hizi mbili zinaamini kuwa safari ya kuelekea katika uchumi usiotegemea matumizi ya pesa taslimu ni suala ambalo linaweza kufikiwa na ni hatua muhimu kwenye uchumi wa Tanzania na zinatumaini kuwa ushirikiano huu utakuwa na mchango chanya kwa Maisha ya Watanzania.

No comments:

Post a Comment