Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 19 May 2020

BENKI YA COMMERCIAL BANK OF AFRICA (CBA) YATOA MSAADA WA MATANKI YA MAJI KWA HOSPITALI ZA UMMA JIJINI DAR ES SALAAM

Mwakilishi kutoka kitengo cha Ugavi wa Hospitali ya Mwananyamala, Hiltruda Patrick (kushoto) akipokea matanki ya maji kutoka kwa Geofrey Kivamba wa Brandmiles kwa niaba ya Benki ya Commercial Bank of Africa (CBA) Tanzania ikiwa ni sehemu ya msaada wa matanki nane ya maji yasiyo na mkono kwa hospitali nne zilizochaguliwa jijini Dar es salaam ili kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka ya kusafisha mikono ambayo ni hatua muhimu katika kupambana na COVID-19. Katikati ni Mfamasia wa hospitali hiyo, Simon Mbise.



15 Mei 2020, Dar es Salaam - Benki ya Commercial Bank of Africa (CBA) Tanzania imetoa msaada wa matanki nane ya maji yasiyo na mkono kwa hospitali nne zilizochaguliwa jijini Dar es salaam kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka ya kusafisha mikono ambayo ni hatua muhimu katika kupambana na COVID-19.

Akikabidhi mchango huo Afisa Mtendaji Mkuu wa CBA, Gift Shoko amesema msaada huo ni sehemu ya hatua zilizochukuliwa na CBA kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na kusambaa kwa COVID-19 nchini Tanzania.

"Commercial Bank of Africa (Tanzania) imejitolea kusaidia hospitali ziweze kutoa vifaa sahihi kwa watu wanaotembelea hospitali hizo ili kuwawezesha kutekeleza utaratibu wa kunawa mikono kwa sababu ni silaha muhimu ya kupambana na virusi vya corona. Mara baada ya kutambua kuwepo kwa ongezeko la mahitaji ya vifaa vya kunawia mikono, benki ya CBA ilianza kufanya mchakato wa kupata matanki kwaajili ya kuhifadhia maji katika kusaidia upatikanaji wa vifaa vya kunawia mikono katika hospitali ambako ndio sehemu muhimu kwaajili ya ustawi wa jamii ya Dar es salaam." Alifafanua bwana Shoko

"Kama tunavyofahamu, maambukizi ya virusi vya corona yanaweza kutokea kwa kugusa sehemu iliyoguswa na mtu mwenye virusi, hivyo tumehakikisha kwamba matanki ya maji yamewekewa kifaa cha kufungulia maji kwa kukanyaga kwa mguu ili kumlinda zaidi mtumiaji.

Hospitali ambazo zimenufaika na msaada huo ni pamoja na Amana, Sinza, Mwananyamala na Lugalo.

Hospitali hizi zinahudumia idadi kubwa ya watu kila siku, hivyo tuliamua kuanza na hizi. Ni matumaini yetu kwamba tutaweza kuzifikia hospitali nyingi zaidi katika siku zijazo"
Alieleza zaidi bwana Shoko.


Ili kukuza ufahamu kuhusu Virusi vya Corona miongoni mwa wateja, benki ya CBA imeweka taarifa katika mfumo wa barua pepe, ujumbe mfupi wa maneno, mabango pamoja na kutumia mitandao ya kijamii (Facebook na Twitter) kutuma ujumbe wenye taarifa sahihi kwa umma kuhusu COVID-19 ni nini na ni jinsi gani ya kujilinda, Kujikinga na kuchukua hatua.

"Benki ya CBA imeweka kipaumbele kikubwa katika usalama wa wafanyakazi wake na wateja kwa kuweka dawa za kusafisha mikono (hand sanitizers) katika milango na katika vyumba ili ziweze kufikiwa na kutumiwa kwa urahisi na wafanyakazi wetu. Iwapo itatokea dharura benki ya CBA imeandaa vyumba maalumu kwaajili ya kushughulikia matukio ya dharura wakati msaada wa kitabibu unafuatiliwa, hii ni kwa Makao Makuu pamoja na katika matawi yetu yote nchi nzima", alihitimisha Shoko.

Vile vile benki ya CBA imeweka mfumo kwaajili ya idara ambazo sio lazima ziweko ofisini kuweza kufanya kazi nyumbani kwa kutumia vifaa vya kidigitali vya mawasiliano na uendelevu wa biashara kwa lengo la kupunguza safari na hatari ya kusambaa kwa COVID-19.

Kuhusu Benki ya Commercial Bank of Africa Tanzania- CBA Benki ya CBA Tanzania ni benki tanzu ya kundi mama la mabenki ya Commercial Bank of Africa Ltd ambalo limekuwa linaendesha shughuli zake kwa zaidi ya miaka 50, Benki ya CBA Tanzania ni watoa huduma za kifedha wenye ubora wa viwango vya kimataifa. Ikiwa inawapatia wateja wake aina mbalimbali za bidhaa na huduma ambazo zimeandaliwa mahususi kukidhi mahitaji ya ndani ya nchi na ambazo zimetokana na uvumbuzi wa kimataifa.

Pamoja na ndoto ya kuwa watoa huduma za kifedha wakubwa na wanaoheshimika Afrika Mashariki na Malengo ya kukuza utajiri na utilimifu wa maisha kwa wateja wetu, benki ya CBA Tanzania vile vile inalengo la kuwapatia wateja huduma za kifedha za kipekee ambazo zinawawezesha kuhifadhi fedha, kuwekeza na kukuza utajiri ambazo zimeijengea sifa benki hii kuwa ndio benki tegemeo kwa mashirika, taasisi, mikakati ya kidiplomasia, NGOs na wateja binafsi wenye thamani ya juu.

Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na:
Commercial Bank of Africa Limited,
Ohio Street, Amani Place,
Dar es Salaam, Tanzania.
Simu: +255222130113
Faksi: +255222130116
Barua Pepe: contact@cbagroup.com

No comments:

Post a Comment