Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 11 October 2019

BENKI YA LETSHEGO YAZINDUA AKAUNTI YA LETSGO FLEXI

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Letshego Tanzania, Andrew Tarimo (aliyekaa kulia) akimhudumia mteja katika maadhimisho ya wiki ya wateja. Benki hiyo imezindua akaunti maalum ya LegtsGo Flexi ambapo wateja watapata riba ya asilimia kumi kwa mwaka kwa kuweka kiasi cha fedha cha kuanzia Tzs50,000.
  • Wateja kupata hadi riba ya asilimia 10 kwa mwaka
Dar es Salaam. 11 Oktoba 2019: Watanzania watakiwa kujenga utaratibu wa kujiwekea akiba ili kuimarisha uchumi wa familia na nchi kwa ujumla ili kufikia malengo ya kujenga uchumi wa viwanda. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Biashara wa Letshego Bank, Solomon Haule alipokutana na wateja wa Bank hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma ya LetsGo Flexi save akauntiHii ni akaunti ya akiba inayotoa faida ya riba hadi asilimia kumi kwa mwaka kulingana na akiba ya mteja.

"LetsGo Flexi save ni akaunti jumuishi kwa sababu imezingatia na kuweka mbele maslahi ya wateja wote bila kuangalia uwezo au kipato cha mtu kupitia akaunti hii hata wateja wadogo wenye akiba chini ya shiling 20,000 watapata riba ya hadi asilimia 5% kwa mwaka."


Hafla hiyo pia iliambatana na uadhimishaji wa wiki ya huduma kwa wateja ambapo Letshego Bank ilipata nafasi ya kuwashukuru baadhi ya wateja wao wanaoendelea kuwaunga mkono.

No comments:

Post a Comment