Mheshimiwa Sauda Salum Mtondoo, mkuu wa Wilaya ya Kilindi akikabidhi mabati yaliyotolewa na BancAbc kwa walimu wa shule ambazo zimenufaika na msaada huo. |
Sisi BancABC tunaamini kwenye umuhimu wa elimu bora katika jamii zetu hapa Tanzania na kwa hivyo tunaunga mkono Serikali ya Awamu ya 5 na hususani Rais wetu Mhe. John Pombe Mafuguli katika miradi mbali mbali ya elimu kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu na kuweza kuwafikia kila jamii na hasa maeneo ya vijijini kwa wale ambao wako kwenye hali duni.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi Bw. Emmanuel Nzutu ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi alisema; “Kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa elimu bure kwa kila Mtanzania kuanzia chekechea hadi kidato cha nne, Leo Bancabc tunatoa msaada wa mabati 200 kwa wilaya ya Kilindi, na msaada huu tunaukabidhi hapa kwa Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Sauda Salum Mtondoo.”
Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha Bancabc na pia kuwajulisha kuwa benki yetu tunatoa huduma ya Mkopo ambao ni mahususi kwa wafanyakazi wa serikali, Easy loans ambapo inakupa nafasi ya kulipa Mkopo kwa muda wa miaka sita na vile vile una uwezo wa kuweza kuongeza Mkopo hata kabla ya kumaliza kulipa ule wa awali.
Uzuri wa mkopo huu tofauti na mikopo mingine ni kwamba, mwenye kuomba Mkopo anaweza kuchagua ni mradi gani wa kuwekeza fedha zake kwa mfano kulipa karo ya shule, kununua gari, kufanya marekebisho ya nyumba, kulipa kodi ya nyumba au kumalizia ujenzi.
Vile vile tunaweza kununua Mkopo wako wa awali ukabaki na Mkopo mpya.
‘Mkopo huu utakuwa na bima ya maisha pale ambapo mwenye Mkopo anapofariki, familia yake inapewa pesa taslimu Tzs500,000 kwa ajili ya kugharamia mazishi.’
Tunatoa wito kwa wateja wetu na wale ambao pia sio wateja wetu kujiunga na Bancabc na kuchangamkia Mkopo huu kwani sisi tunakuweka karibu na ndoto zako.
No comments:
Post a Comment