Kampuni ya Tigo hivi karibuni imezindua duka jipya la huduma kwa wateja lililopo Iringa mjini ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wake wa eneo la Iringa mjini na maeneo ya jirani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo Mkurungezi wa kanda ya Kusini wa Tigo, Henry Kinabo, amesema tawi hilo jipya lililopo mtaa wa Miyomboni, ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kuwafikishia wateja wake huduma zake karibu zaidi.
Kinabo alisema duka hilo litahudumia wateja zaidi ya 100 kwa siku kwa kuwapa huduma mbalimbali za Tigo ikiwemo huduma ya kuunganishwa na intaneti, usajili wa laini za simu, Tigo Pesa na huduma za simu janja.
“Duka hili lina manufaa makubwa kwa wateja kwa sababu imepeleka huduma zetu kuwa karibu zaidi na wao. Pia linapatikana sehemu nzuri inayofikika kirahisi kiasi kwamba litavutia wateja wengi kutoka maeneo jirani. Tumebadilisha pia muonekano wa duka letu kuwa mzuri zaidi, na kuongeza pia nafasi ili kuweza kuwahudumia wateja wengi zaidi kwa wakati mmoja,” alisema.
Aliongeza, “Kupitia duka letu hili lililoboreshwa, wateja watapata pia promosheni zetu mbali mbali kama; 4G+, App ya Tigo Pesa, promosheni ya CASH INkwa mawakala, pamoja na simu mpya za S10 na S10+.”
Duka hili limetenga pia sehemu maalum ya uuzaji wa bidhaa mbalimbali kama simu janja ambapo mteja anaruhusiwa kuzijaribu kabla ya kununua. “Hii inamuwezesha mteja kufanya uamuzi sahihi kabla ya kununua, hivyo huchagua na kununua aina ya simu inayokidhi mahitaji yake.”
No comments:
Post a Comment