Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 15 February 2019

BENKI YA NBC YACHANGIA UJENZI WA KITUO CHA POLISI RUANGWA MKOANI LINDI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa pili kushoto), akipokea mfano wa hundi ya Shilingi 11,270,000 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, kwa ajili ya kununulia mifuko 1,000 ya saruji kama mchango wa NBC kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi cha Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi. Hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
DAR ES SALAAM. 14 FEBRUARI 2019 - BENKI ya NBC imetoa msaada wa mifuko 1,000 ya saruji kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi cha Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

Msaada huo umekabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ofisi zake Ikulu jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi amesema NBC ni Benki ya Wazalendo na tunajiona fahari kuweka juhudi zetu katika kuhakikisha kila mwananchi na mzalendo wa Taifa letu anaishi kwa usalama na utulivu.

“Kama taasisi ya fedha ni imani yetu kuwa Jeshi la Polisi likiwezeshwa kwa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo majengo ya vituo pamoja na makazi ya askari litaweza kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa ufanisi ambayo ni kulinda usalama wa raia na mali zao.

Benki ya NBC inajua pia eneo litakalojengwa kituo hiki wapo wateja wetu na wale wateja watarajiwa hivyo ujenzi wa kituo hiki utasaidia sana kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo hivyo kuwafanya wakazi wake kuzalisha mali katika hali ya utulivu hiyvo kukuza uchumi wao na wa Taifa.

“Benki ya NBC inapenda kutoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli kwa jitihada zake katika kujenga mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili kwa pamoja kutimiza azma ya kuelekea Tanzania ya viwanda.

Utulivu na amani uliopo nchini ni moja ya sababu kubwa ya mafanikio na maendeleo ya benki yetu ambayo sasa imetimiza zaidi ya miaka 50 ikiendelea kuwa moja ya taasisi kubwa ya fedha na yenye nguvu katika kuwatumikia wananchi.

About NBC;

NBC is one of the most represented retail banks in the country with over 50 years’ experience in providing financial services. Apart from offering traditional banking services, NBC also prides itself on an expanded branch network of 51 branches and over 220 Visa enabled ATMs. The bank also services over 150 Points of Sales strategically located throughout the country. NBC employs over 1,200 staff.

No comments:

Post a Comment