Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 29 November 2018

WAFANYAKAZI WA BENKI YA NBC WAJITOLEA DAMU KUCHANGIA WENYE UHITAJI

Mkurugeni Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akizungumza na waandishi wa habari akielezea jinsi wafanyakazi wa benki hiyo walivyoguswa katika kujitolea damu kwa ajili ya watu wenye uhitaji.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC wakijitolea damu ili kusaidia wenye uhitaji kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Hazina na Masoko ya Fedha wa NBC, Peter Nalitolela akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu zoezi hilo. NBC imeandaa zoezi hilo kwa muda wa siku tatu ambapo wafanyakazi wake watashiriki katika uchangiaji wa damu kwa hiari.
Mmoja wa Wafanyakazi wa NBC, Salama Mussa (kulia), akipimwa damu yake ili kuona kama inakidhi vigezo vya kujitolea damu katika hafla hiyo. Anayempima ni mhudumu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Ndonya Hussein.
Mmoja wa wafanyakazi wa NBC, Jeff Ndossa (kulia), akijitolea damu ili kusaidia wenye uhitaji kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama katika hafla iliyoandaliwa na NBC jijini Dar es Salaam jana. Anayemtoa damu ni mhudumu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Ali Juma.
Mfanyakazi wa NBC, Basil Kihanga (kushoto), pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakijitolea damu ili kusaidia wenye uhitaji kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mmoja wa wafanyakazi wa NBC, Saidi Bakari akiwa katika hatua za maandalizi ya utoaji wa damu katika hafla hiyo. Kushoto ni Ndonya Hussein kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama. 
Mhudumu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Ndonya Hussein (kushoto), akichukua sampuli ya damu kutoka kwa mfanyakazi wa NBC, Suzyo Gwebe Nyirenda katika zoezi la uchangiaji damu liliandaliwa na NBC jijini Dar es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment