Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 28 September 2018

NBC MDHAMINI MKUU MAONYESHO YA MADINI GEITA

Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe ( kushoto), akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) wakati naibu waziri huyo alipokwenda kuzindua rasmi maonyesho ya kwanza ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini Mkoani Geita juzi. NBC ilikuwa ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo. Wengine kulia kwa naibu waziri ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Robert, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonyesho, Chacha Wambura na Meneja wa NBC Geita, Martin Nkanda.
Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (wa pili kushoto), akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) wakati naibu waziri huyo alipokwenda kuzindua rasmi maonyesho ya kwanza ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini Mkoani Geita juzi. NBC ilikuwa ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo. Wengine kutoka kulia ni Meneja wa NBC Geita, Martin Nkanda, Meneja wa Kanda ya Ziwa, Japhet Mazumira na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati, Evance Luhimbo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Robert (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wapili kulia) na Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe wakitembelea moja ya mabanda ya wajasiriamali katika maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini mjini Geita hivi karibuni. NBC ilikuwa ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo.
Ofisa wa Huduma kwa wateja wa Benki ya NBC, Pili Salum akizungumza na watoto wa Shule ya Msingi Nyanza wakati wa maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya CCM Kalangalala mkoani Geita.
Ofisa Mahusiano ya Wateja wa Benki ya NBC, Esther Kahabi akizungumza na wakazi wa Geita pamoja na wafanyakazi wa migodini wakati wa maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita.
Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Benki ya NBC, Japhet Mazumira (kushoto) akizungumza na kikundi cha wajasiriamali wadogo wadogo mafundi viatu walemavu baada ya kutembelea katika banda lao wakati wa maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mkoani Geita. 
Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Joseph Boaz (kulia) akizungumza na wakazi wa Geita pamoja na wafanyakazi wa migodini wakati wa maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita.

No comments:

Post a Comment