Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 28 September 2018

AIRTEL YAWEKEZA KATIKA MADUKA YA KUTOA HUDUMA NCHI NZIMA

Mkuu Wa mauzo wa Airtel Dar es salaam, Bryton Majwala akiongea na baadhi ya wateja wakati wa kuzindua moja kati ya maduka madogo madogo ya Airtel maarufu kama Airtel Money Branch mkoani Dar es salaam Mbezi Tangi bovu ambapo zaidi ya maduka 400 yameshafunguliwa katika maeneo mbalimbali nchini. Anaehudumia wateja ni Afisa huduma kwa wateja wa duka hilo la Airtel Money Branch Tangi Bovu Bw, Thobias Bango. Duka hilo la Airtel limezindualia rasmi jana na Airtel ambapo litatoa huduma zote za Airtel kama vile kuweka na kutoa pesa –Airtel Money, kurejesha laini iliopotea na kuharibika, pamoja na kusajili laini mpya kwa wateja wapya.
Afisa huduma kwa wateja wa Airtel Branch ya Mbezi Tangi Bovu bw, Thobiasi Bango akitoa huduma ya kusajili laini mpya kwa wateja wa kwanza kwenye duka hilo mara baada ya uzinduzi wa duka hilo, Duka hilo la Airtel Money Branch Mbezi Tangibovu ni moja kati ya maduka 400 yaliyofunguliwa nchini na Airtel ikiwa ni mkakati wake wa kufikisha huduma zao kila mahali, huduma zinazotolewa ni pamoja na le kuweka na kutoa pesa –Airtel Money, kurejesha laini iliopotea na kuharibika, pamoja na kusajili laini mpya kwa wateja wapya.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando (wa kwanza kulia) pamoja na msimamizi wa duka la huduma kwa wateja la Airtel Money Branch la Mbezi Tangi Bovu Thobias Bango wakisajili laini ya mteja wa kwanza Bi Elizabeth Gundula mara baada ya uzinduzi wa duka hilo jana. Duka la Airtel Money Branch Mbezi Tangibovu ni moja kati ni ya mikakati wa Airtel wa kufikisha huduma kila mahali, katika maduka hayo mteja ataweza kuweka na kutoa pesa –Airtel Money, kurejesha laini iliopotea au kuharibika au kusajili laini mpya kwa wateja wapya.
Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel, inaendelea na mpango wake wa kuboresha huduma zake, ambapo kwa sasa imekuja na mipango ya kufungua maduka yanayotoa huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo ikiwa ni hatua ya kusogeza huduma hizo kwa wananchi.

Katika kutekeleza mpango huo, tayari Airtel imefungua maduka zaidi ya 400 katika maeneo mbalimbali Nchini na hivyo kusogeza karibu na wateja wake huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutuma na kupokea pesa, kurudisha namba iliyopote, kuswap Sim Card na kununua vifurushi mbalimbali vya Airtel.

Akizungumzia mpango huo wa kufungua maduka na kutoa huduma kwa Mkoa wa dare s Salaam, Meneja wa Biashara Airtel Mkoa wa Dar es Salaam, Brighton Majwala amesema, miongoni mwa maduka yoa ya mkoa wa Dar es Salaam yamewezesha wateja wao kupata huduma za kampuni hiyo kwa urahisi zaidi.

“Sisi Airtel, tumeamua kuanzisha maduka haya ili kusogeza karibu huduma zetu kwa lengo la kuwawezesha wananchi na wateja wetu kupata huduma hizo kwa urahisi na pia karibu na maeneo yao,” amesema Majwala.

“Hata hivyo hii ni fursa ya kipekee kwa mawakala wetu kuweza kupata huduma za Airtel Money na huduma nyingine bila kutembea umbali mrefu kuzifuata kama ilivyokuwa hapo awali”. ameongeza.

Kwa upande wao baadhi ya wateja na mawakala wa wa Kampuni hiyo, wameeleza namna ambavyo wananufaika na huduma zinazotolewa na maduka hayo ya Airtel katika maeneo yao.

“sisi wateja, tunafurahia huduma hizi kusogezwa karibu na maeneo yetu kwani inaturahisishia kupata huduma na kuokoa muda ambao tungeutumia kufuata huduma hizo maeneo mengine ya mbali na hapa” walieleza wateja hao.

“Mawakala wengi wa hapa maeneo ya Tangi Bovu tunanufaika sana na uwepo wa Duka hili la Airtel katika maeneo yetu kwani kwa sasa tuweza kumuhudumia mteja kiasi chochote cha Airtel Money bila kuhangaika kufuata floti maneo ya mbali” aliongeza wakala Elizabeth Madeje

Kufunguliwa kwa maduka hayo katika maeneo ya karibu na wananchi, kumeelezwa kuwasaidia wananchi na wateja wa Airtel kupata huduma za kampuni hiyo kwa urahisi na hivyo kuokoa fedha na muda wa kufuata huduma hizo maeneo ya mbali.

No comments:

Post a Comment