Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 21 December 2017

QNET YATOA ZAWADI YA SIKUKUU KWA WATOTO YATIMA

Mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki (kulia) akikabidhi mashine ya kusafishia maji ya kunywa (water purifier) pamoja na mahitaji mengine ya kibinadamu kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki akikabidhi misaada mbalimbali ikiwepo vyakula na mahitaji muhimu ya kibinadamu kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam.
Tarehe 20th Desemba, Dar es salaam – Moja kati ya taasisi inayokua kwa kasi sana Tanzania ya masoko ya mtandao QNET, leo imetoa msaada wa mashine yenye mfumo wa kusafisha maji ya Water purifier na chakula chenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2 kwa kituo cha watoto yatima cha Khayraat jijini Dar es salaam.

Msaada wa QNET ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo za kuwajibika katika jamii, ambazo zimeelekezwa katika kutoa msaada wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa zaidi ya watoto 500 wenye uhitaji katika kituo cha kulelea watoto yatima na kuwapatia chakula kwaajili ya kuwawezesha kufurahia sikukuu za krimasi katika kipindi hiki cha sikukuu kama watoto wengine.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa QNET Tanzania Benjamin Mariki, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ina sera bora ya uwajibikaji kwa jamii ambayo inatafuta kutoa kwa jamii inayoihudumia.

“Katika kampuni ya QNET, tunaamini kuwa zaidi ya kusambaza bidhaa zenye ubora wa kiwango cha juu kwa wateja wetu, tuna jukumu la kusaidia serikali na wadau wengine katika kutekeleza shughuli ambazo zina athari nzuri kwa jamii, hasa miongoni mwa wanajamii wenye uwezo mdogo,” alisema Mariki.

Mariki alisema kuwa msaada uliotolewa kwaajili ya kituo ni pamoja na ufungaji wa mashine ya kusafishia maji, kilo 100 za Mchele, kilo 100 za maharage, kilo 100 za unga, lita 60 za mafuta ya kupikia, kilo 100 za sukari, kilo 100 za sabuni ya kufulia pamoja na biskuti, pipi na juisi.

Akipokea msaada huo, Mwasisi wa kituo cha Khayraat Orphans Centre, Bi Khadija Khussein aliishukuru kampuni ya QNET kwa kutoa msaada akisema kuwa msaada huo utawasaidia kwa kiwango kikubwa watoto walioko kituoni.

“Tunashukuru kwa msaada huo tukiwa tunatambua kuwa mashine ya kusafishia maji ya water purifier itasaidia katika kurahisisha upatikanaji wa maji safi na salama kwaajili ya watoto, hivyo kutoa uhakika wa afya kwa watoto kwa kuzuia magonjwa yanayoambukizwa kwa maji kama vile typhoid na Kipindupindu wakati vyakula vitawapa watoto nafasi ya kufurahia sikukuu ya krimasi na mwaka mpya”. Alibainisha Bi Khussein

Kuhusu QNET
Ni kampuni maarufu ya mauzo ya moja kwa moja yenye asili ya Asia, QNET inatoa aina mbalimbali za bidhaa za kuboresha maisha ambazo zinatolewa kupitia mfumo wake wa biashara ya mtandao (e-commerce) kwa wateja na wasambazaji katika zaidi ya nchi 100. Kampuni hii pia ina baadhi ya ofisi zake na Mawakala katika nchi 25 duniani kote, na zaidi ya watayarishaji 50, nje ya waendeshaji wa ndani ya nchi au mawakala katika nchi kadhaa.

QNET ni mwanachama wa Chama cha wauzaji wa moja kwa moja (Direct Selling Association) cha Malayasia, Singapore, Ufilipino na Indonesia. QNET pia ni sehemu ya Chama cha Chakula Bora cha Hong Kong (Hong Kong Health Food Association) na Chama cha viwanda vya Virutubisho vya afya cha Singapore (Health Supplements Industry Association) miongoni wa vingine.

QNET pia inafanya vizuri katika kudhamini michezo dunia kote, ikijumuisha mpira wa miguu (Mshirika wa moja kwa moja wa mauzo wa Klabu ya Manchester City), Mashindano ya Magari ya fomula One, badminton na zaidi, kufuatia imani thabiti ya kampuni ya QNET kwamba msukumo, ari na kufanya kazi kwa pamoja katika michezo kunaendana na ule wa QNET

Kwa maelezo zaidi kuhusu QNET, Tafadhali tembelea Wavuti ya QNET, www.qnet.net

No comments:

Post a Comment