Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 13 July 2017

ECOBANK, TICTS ZAJIPANGA KURAHISISHA HUDUMA BANDARINI

Dar es Salaam. Benki ya Ecobank imesaini makubaliano na Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Shehena za Kontena Bandarini (Ticts) ili kurahisisha ulipiaji wa mizigo kwa watumiaji wa Bandari ya Dar es Salaam. 

Hatua hiyo imeelezwa itaongeza ufanisi na kuwavutia watu wengi zaidi kutumia bandari hiyo kwa kuwa mizigo itatolewa kwa haraka zaidi. 

Akizungumza leo, Julai 11 wakati wa kusaini makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Ecobank, Raphael Benedict amesema hatua hiyo itapunguza muda wa kupata kibali kwa kuwa hakutakuwa na usumbufu.

Katika huduma hiyo, mteja wa Ticts  anaweza kulipia mizigo au makontena akiwa nje ya nchi kupitia matawi zaidi ya 36 duniani. 

"Tumeangalia ni changamoto zipi zinawapata wateja na kuja na suluhisho la kujenga mfumo ili wateja waweze kufanya malipo yao kwa urahisi zaidi," amesema Benedict.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Ticts nchini, Jered Zerbe amesema huduma hiyo ni muhimu kwa kuwa itapunguza gharama za kutuma fedha na itaboresha mazingira ya biashara. 

Amsema pia itaongeza ufanisi katika kulipia kodi ya mizigo inayoingia nchini. 
Meneja Malipo wa Ecobank, Isaac Kamuta amesema mbali na kurahisisha malipo hatua hiyo itawaondolea gharama zisizo za lazima zitokanazo na kuchelewa kutoa mizigo bandarini. 

Kwa sasa huduma hiyo itafanyika kupitia matawi ya benki hiyo lakini itapanua wigo zaidi ili kuwezesha kutumia simu. 

"Hii itarahisisha katika uboreshaji wa huduma katika Bandari ya Dar es Salaam. Mtu akiagiza mzigo akiwa Congo, analipia invoice (stakabadhi ya malipo) na zitaonekana Ticts," amesema.

No comments:

Post a Comment