Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 19 August 2016

BENKI YA CRDB IMEKANUSHA VIKALI HABARI KWAMBA IMESIMAMISHA MIKOPO KUTOKANA NA "HALI TETE YA UCHUMU WA NCHI"

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei.
Benki ya CRDB imekanusha vikali habari iliyoandikwa jana Agosti 18, 2016 na gazeti moja la kiswahili la kila siku na kunukuliwa na baadhi ya mitandao ya kijamii na kumnukuu kimakosa Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Charles Kimei (pichani) kuwa Benki hiyo “Sasa imesimamisha mikopo kutokana na "hali tete ya uchumi wa nchi ".

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB Bi. Tully Esther Mwambapa, amekanusha vikali habari hiyo ambayo ameitaja kuwa inalenga kuwatia hofu wateja wao wapendwa na kuichonganisha Benki ya CRDB na dola. “Nachukua fursa hii kuwatangazia wateja wetu na watanzania wote kwa ujumla kuwa waipuuze taarifa hii na kuwajulisha kuwa Benki inatoa mikopo kama kawaida na tunawakaribisha kuja kukopa ili kwa pamoja tujenge uchumi wa taifa letu”, amesema Bi. Mwambapa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo.

Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment